Katika hatua ya kufariji kwa harakati za kiteknolojia hapa nchini, timu ya vijana wa Kitanzania wametoa programu mpya ya kufuatilia ligi kuu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara – Vodacom Ligi Kuu Bara.
Programu hiyo inayoitwa Soka ilingia kwenye soko la programu ya Google Play Store kwa simu za mkonono mwishoni mwa mwezi Octoba na hadi sasa imepakuliwa zaidi ya mara 500.
Soka ni programu ya kipekee ya aina yake kwa sasa na inawapa mashabiki wa mpira wa miguu na ligi kuu bara urahisi wa kuona mechi zilizopangwa, msimamo wa ligi, timu zinazoshiriki na taarifa zao muhimu, taarifa za vikosi na wachezaji kupitia simu-janja kama anavyoeleza Musa Kalokola, mmoja wa watengenezaji wa SOKA kama inavyoripotiwa na gazeti la The Citizen.
Wakiongea katika hatua tofauti, Michael Kimollo, Noel Sumbe, Memory Mwageni na Mathias Charles wanaelezea pia hatua mbalimbali walizopitia katika safari nzima ya kutengeneza programu hiyo ikiwemo changamoto za mwanzo na shirikisho la mpira TFF ili kupata ruhusa ya taarifa za timu na wachezaji, uvumilivu na teknolojia, bidii na umoja ingawa wametoka vyuo tofauti na mchango mkubwa wa uongozi wa BUNI iliyoko katika jengo la COSTECH.
Programu ya SOKA ni rahisi kutumia na ni hatua nzuri ya kutengeza teknolojia ya watanzania kwa mambo ya kitanzania. Kuipakua Soka kwenye androidi, fuata linki hii ->> Google Play
No Comment! Be the first one.