Mambo mengi sana yamebadilika toka mwaka 2007 ambapo kampuni la Apple lilizindua simu janja yake ya kwanza katika mtiririko wako wa iPhone. Simu hii ililibadilisha kampuni na soko la simu janja kwa ujumla
Mpaka sasa kampuni lina simu zenye sifa za aina yake na zimeteka kabisa soko la simu janja. Ukiachana na kuteka soko hili, simu hizi zimetoka mbali sana. Leo TeknoKona ipo tayari kukupati matoleo yote ya simu za iphone toka mwaka 2007 ili ujionee hatua iliyopigwa na kampuni hili
1. iPhone (iPhone 2G)
Cha Kuvutia: Hii ndio simu ilibadilisha soko zima kwa ujumla, simu hii iliwafungua macho watumiaji wa simu za kawaida na soko la simu janja likaanza kupanuka kuwa kubwa zaidi.
Uwezo Wa Kamera: 2 Megapixel
Bei Ya Kwanza Kabisa: 4GB – $499, 8GB – $599 (Dola za Kimarekani)
Idadi Ya App Kutoka Nje Ya Kampuni: 0
2. iPhone 3G
Cha Kuvutia: Iliyokuwa na uwezo mzuri wa netweki ambayo haitumii nyaya (wireless) na pia hii ndio ilianzisha matumizi ya App mbalimbali kwa bei ya chini
Kipya: App Store,Picha kujihifadhi huku zikionyesha maeneo zilipopigiwa (Photo geotagging) n.k
Uwezo Wa Kamera: 2 Megapixel
Bei Yake Ya Kwanza: 8GB – $499, 16GB – $599, 32GB – $699
Idadi Ya App Kutoka Nje Ya Kampuni: 500
3. iPhone 3GS
Cha Kuvutia: Ilikua na spidi katika ufanisi na utumiaji mdogo wa betri. Vipengele vyake vikubwa vilikuwa ule uwezo wake wa kukata, kunakili na ku ‘paste’ (Cut, Copy & Paste) maneno.
Kipya: Uwezo wa kutafuta (search), kukata, kunakili na ku ‘paste’ (Cut, Copy & Paste maneno, Keyboard inayolala kama ukilaza simu (Landscape keyboard)
Uwezo Wa Kamera: 3 Megapixel
Bei Yake Ya Kwanza: 16GB – $649, 32GB – $749
Idadi Ya App Kutoka Nje Ya Kampuni: 50,000
4. iPhone 4
Cha Kuvutia: Muundo wake kwa ujumla ambao una madini ya chuma na kioo pamoja na uanzilishi na huduma ya video ya FaceTime
Kipya: FaceTime, Kamera ya megapixel 5, iBook na uwezo wa HD katika kurekodi video
Uwezo Wa Kamera: 5 Megapixel
Bei Yake Ya Kwanza: 16GB – $649, 32GB – $749
Idadi Ya App Kutoka Nje Ya Kampuni: 225,000
5. iPhone 4S
Cha kuvutia: Programu endeshaji mpya (iOS 5). Huduma mpya kama vile iCloud na iMessege
Kipya: iMessege, Prosesa ya ‘A5 Dual core’
Uwezo Wa Kamera: 8 Megapixel
Bei Yake Ya Kwanza: 16GB – $649, 32GB – $749, 64GB – $849
Idadi Ya App Kutoka Nje Ya Kampuni: 360,000
6. iPhone 5
Cha Kuvutia: program endeshaji mpya (iOS 6). Maboresho ya vipengele mbalimbali kama vile App ya Map, Njia mpya yak u ‘Scan’ vitu kama vile tiketi,kuponi n.k
Kipya: Kioo cha inchi 4 (simu za nyuma zilikuwa na inchi 3.5). kuuongezeka kwa kioo hichi kiliwezesha simu kuwa na mistari mingi yenye ‘icon’ (mstari wa 5) katika uwanya wake wa nyumbani (home screen)
Uwezo Wa Kamera: 8 Megapixel
Bei Yake Ya Kwanza: 16GB – $649, 32GB – $749, 64GB – $840
Idadi Ya App Kutoka Nje Ya Kampuni: 700,000
7. iPhone 5C
Cha Kuvutia: imekuja na rangi nyingi kuliko matoleo mengine ya iPhone. Inapatikana kwa rangi Nyeupe, Njano, Bluu, Kijani na Pinki.
Kipya: Imekuja na programu endeshaji ya iOS 7. Kioo cha inchi 4
Uwezo Wa Kamera: 8 Megapixel
Bei Yake Ya Kwanza: 16GB – $549, 32GB – $649
Idadi Ya App Kutoka Nje Ya Kampuni: 900,000
8. iPhone 5S
Cha Kuvutia: Prosesa yenye chipu ya A7, ambayo inafanya kazi haraka zaidi. Muonekano wake ni mwembamba na ni nyepesi. Inapatikana kwa rangi tatu; gold , silva na gray (kama kijivu flani hivi kinaenda kwenye weusi)
Kipya: Inauwezo wa kusensi vidole (fingerprint). 5s imekuja na program endeshaji ya iOS 7.
Uwezo Wa Kamera: 8 Megapixels
Bei Yake Ya Kwanza: 16GB – $649, 32GB – $749, 64GB – $849
Idadi Ya App Kutoka Nje Ya Kampuni: 900,000
9. iPhone 6
Cha Kuvutia: Prosesa mpya yenye chipu ya A8 ambayo inafanya kazi zaidi ya 80% kulinganisha na iPhone ya kwanza kabisa.
Kipya: Kioo cha inchi 4.7, Uboreshwaji wa kamera ya mbele,Teknolojia ya Near-fueld communication (NFC) na mfumo mpya wa Apple Pay kuwekwa
Uwezo Wa Kamera: 8 Megapixel
Bei Yake Ya Kwanza: 16GB – $649, 64GB – $749, 128GB – $849
Idadi Ya App Kutoka Nje Ya Kampuni: Milioni 1.3
10. iPhone 6 PLUS
Cha Kuvutia: Prosesa mpya yenye chipu ya A8 ambayo inafanya kazi zaidi ya 80% kulinganisha na iPhone ya kwanza kabisa.
Kipya: Kioo cha inchi 5.5, Uboreshwaji wa kamera ya mbele,Teknolojia ya Near-fueld communication (NFC) na mfumo mpya wa Apple Pay kuwekwa
Uwezo Wa Kamera: 8 Megapixel
Bei Yake Ya Kwanza: 16GB – $749, 64GB – $849, 128GB – $949
Idadi Ya App Kutoka Nje Ya Kampuni: Milioni 1.3
11. iPhone 6S
Cha Kuvutia: Uwezo Wa tachi ya 3D (3D Touch) ambayo itafanya kazi kulingana na jinsi ulivyogusa kioo cha simu
Kipya: Rangi za upatikani kwa simu hii ni; silva, kijivu, gold na rose gold. Prosesa ya 64- bit ambayo ina chipu ya A9. Uwezo wa kiwango cha 4K HD katika video. FaceTime kuwa na kamera yenye kiwango cha HD ambayo ina 5 Megapixel
Uwezo Wa Kamera: 12 Megapixel
12. iPhone 6S PLUS
Cha Kuvutia: Uwezo wa Tachi ya 3D (3D Touch) ambayo itafanya kazi kulingana na presha ya kidole juu ya skrini
Kipya: Kioo cha inchi 5.5. Prosesa ya 64-bit yenye chipu ya A9. Uwezo wa kurekodi video zenye kiwango cha 4K. FaceTime kupata kamera ya HD yenye Megapixel 5.
Uwezo Wa Kamera: 12 Megapixel
13. iPhone SE
Cha Kuvutia: Jumba la iPhone 5S lakini Uwezo wa iPhone 6S.
Kipya: Mwili mdogo, Uwezo mkubwa. Kioo cha inchi 4. Vipengele vingi katika simu hii vipo katika 6S na 6 Plus kama vile video za 4K n.k.
Uwezo Wa Kamera: 12 Megapixel
Bei Yake Ya Kwanza: Dola 399 – 499 za kimarekani
Kwa mtiririko huu kampuni la Apple limeweza kuleta mabadiliko kwa kiasi kikubwa katika soko zima la simu janja. Mabadiliko haya yanaongeza hadi ushindani baina ya kampuni na kampuni, nani aliteke soko?. Katika mlolongo huu inaonekana dhahiri kabisa kwamba kila kwenye toleo jipya la simu zao kuna jambo jipya ambalo linatofautisha kabisa simu zingine za nyuma. Unaweza otea iPhone mpya (iPhone7) zitakuwa na kitu gani kipya?
Bei zilizopangwa hapo juu zinaweza zikawa tofauti tofauti kulingana na maeneo na muamko wa watu juu ya bidhaa husika