Kampuni ya magari ya Ford inatengeneza kizazi kipya cha magari amabayo yanaweza yakaona usiku bila hata ya kutunia taa. Gari hii itakuwa imepandikizwa na uwezo wa kuona katika giza bila kuwasha taa (Night –vision system).
Watu wengi wamejiuliza juu ya kwanini kampuni hiyo imefikiria kitu cha namna hiyo wakati watu wengi hutegemea taa za magari yao wanapoendesha nyakati za giza (usiku). Jibu ni kwamba kampuni la Ford linataka kujiweka katika mstari wa mbele kwa magari yale yanayotumia teknolojia ya juu zaidi.
Kumbuka tumeshawahi sikia makampuni mengi yakiwa yanfanya kazi katika kuhakikisha yanazalisha magari ambayo yanajiendesha yenyewe. Makampuni yanayojikita na teknolojia hiyo katika magari ni moja na Apple na Google.
Turudi kwa Ford, wao wanasema kutokana na kwamba teknolojia imekua sana – kuna magari ya kujiendesha yenyewe – basi haina budi na wao waje na yale ambayo yanaweza tembea usiku bila ya kuwa na taa. Teknolojia hii itakuwa katika magari yao ambayo yatakuwa yanajiendesha yenyewe.
Ford wanasema magari yanayojiendesha yenyewe yanategemea teknolojia ya tofauti katika betri yake, matumizi ya hali ya juu ya GPS, data zinazotokana na kamera na sense za rada
Ford wao wamekuja mbele zaidi kwa kuongeza Teknolojia inayoitwa ‘Light Ditection And Ranging’ (LiDAR) ambayo yenyewe imejikita sana katika mwanga na rada. Teknolojia hii italiwezesha gari kutengeneza picha na kuweza kuona vitu vinavyozunguka gairi barabarani nyakati za giza
Tazama Video Ya Teknolojia Hiyo Hapa
“Teknolojia ya LiDAR inaliwezesha gari kujiendesha nyakati za giza vizuri tuu kama vile inavyofanya katika nyakati za mwanga (mchana)” – Alisema Jim McBride, mkuu wa kitengo cha teknolojia ya magari ya automatiki ya Ford
Teknolojia hii ya LiNDAR nit tofauti kabisa na macho yetu ambayo hutegemea kwa kiasi kikubwa mwanga ili yaweze kuona vizuri
Hii sio teknolojia peke yake amabayo Ford wanakuja nayo, bali zipo nyingi tuu ukijumuisha hata ile ya taa waliokuja nayo mwaka jana. Taa hizo zilikuwa na uwezo wa kuhisi hatari mbeleni na kulazimu gari kwenda katika upande mwingine
One Comment
Comments are closed.