Teknolojia na biashara ya magari yanayojiendesha yenyewe inakua kwa kasi sana. Tayari makampuni nguli kama vile Google, na Tesla yashafika mbali sana kwenye teknolojia hiyo, na sasa kampuni ya Apple imepata kibali cha kufanyanyia majaribio magari yake pia.
Magari hayo ambayo yanatarajia kuleta ushindani kwa Google na Tesla ambao wamemtangulia Apple katika kujihusisha katika teknolojia na biashara ya magari yanayojiendesha yenyewe ambayo yanaonekana kukubalika.
Magari hayo yatafanyiwa majario katika jiji la California na kwa sheria za jiji hilo ni lazima dereva awepo ndani ya gari wakati wa majaribio ili kama chocohote kikienda mrama aweze kusaidia.
Apple wana imani kwamba teknolojia ya magari yanayojiendesha yenyewe yatasaidia kupunguza msongamano wa magari barabarani lakini pia yatasaidia kuepusha vifo vya watu kutokana na ajali za barabarani. Kibali cha Apple kinahusisha magari yote ya Lexus 2015, RX 450h, hybrid SUVs pamoja na madereva sita.
Katika hali ambayo kampuni nguli kama Apple inataka kufanya vyema imewekwa wazi kwamba wamewekeza sana katika utengenezaji wa magari yanayojiendesha yenyewe pamoja na mafunzo kuhusu mashine
Mbali na Apple kuwa na kibali cha kufanyia majaribio magari yake makampuni mengine pia yana vibali cha kufanya majaribio katika jiji la California ambayo yanajumuisha Ford, BMW, General Motors, Tesla, Volkswagen.
Vyanzo: The Guardian, mitandao mbalimbali.