WhatsApp ni moja kati ya App inayotumika sana katika swala zima la kutuma na kupokea ujumbe siku hizi. Na urahisi wake juu ya kuitumia inaifanya izidi kupendwa na watu.
Moja kati ya maswali au maombi tunayopokea kwa wasomaji wetu ni juu ya kutumia akaunti mbili za WhatsApp katika simu moja. Je hili linawezekana? Kwa kawaida jambo hili haliwezekani ila kwa kutumia ujanja ujanja flani linawezekana
Uko Tayari Kuyajua Maujanja Hayo?
Hapa ntakufundisha njia mbili ambazo unaweza kuchagua kutumia inayokufaa kutegemeana na simu yako
NJIA 1: Kuongeza Watumiaji Wa Simu (User)
Njia hii itakubali kwa wale wanaotumia programu endeshaji ya Android 5.0 (lollipop). Kama simu yako ina toleo hilo fanya yafuatayo
• Ongeza akaunti ya mtumiaji wa pili wa simu yako. Kufanya hivyo nenda katika Settings na kisha User alafu Add User
• Malizia kabisa kujaza maelezo husika kuhusiana na akaunti ya mtu wa pili uliyoitengeneza
• Nenda kwa mtumiaji wa pili (New User) kwa kwenda katika eneo la ‘ Notification’ na kisha katika alama ya New User
• Ukifungua hapo utashangaa simu yako imekuwa kama mpya, ikiwa na mambo yote ambayo imekuja nayo (ikiwa kama mpya vile)
• Sasa Shusha na pakua WhatsApp ukiwa unatumia simu yako kama mtu wa pili (New User)
• Ukishamaliza kuipakua unaweza ukajaza namba yako ya pili ambayo unataka kuitumia
Kwa kufanya hivyo utakuwa una uwezo wa kutumia akaunti mbili za WhatsApp katika simu moja. Ukitaka kwenda kuchati katika akaunti husika unaenda katika eneo la User na kisha unachagua unapotaka. Kwa kutumia njia hii unaweza ongeza akaunti nyingi kadri unavyozidi kuongeza akaunti za watumiaji (user) wa simu yako.
NJIA 2: Kwa Kutumia OGWhatsApp
OGWhatsApp ni njia nyingine pia ambayo inakuwezesha kutumia akaunti mbili za WhatsApp katika simu yako ya Android
Ili kuwezesha kwa kutumia simu hii fuata maelekezo yafuatayo.
• Kwanza kabisa fanya Back Up ya taarifa zako za WhatsApp kufanya hivyo nenda Settings > Chat Settings > Backup Chats
• Kisha futa Data zote za WhatsApp kwa kwenda Settings>apps>WhatsApp>Clear Data.
• Katika simu yako ingia katika eneo la File Manager na tafuta faili la WhatsApp ambalo utalikuta katika folder la /SD Card/Whatsapp. Badilisha jina faili hilo lisomeke /sdcard/OGWhatsApp
• Futa App (uninstall) yako ya WhatsApp katika simu yako
• Sasa Install OGWhatsApp katika simu yako kwa kubofya hapa
• Ukishamaliza kuipakua kumbuka kuhakikisha namba yako ya zamani amabyo ulikua unaitumia katika WhatsApp ya kawaida
• Sasa nenda katika Google play store na kisha Install App ya WhatsApp yenyewe na ikimaliza ingiza namba ya pili ambayo unataka uwe unatumia kama akaunti ya pili
Mpaka hapo nikupe hongera sana! Maana utakuwa umefanikiwa kuwa na akaunti mbili za WhatsApp katika simu moja.
Njia hizi ni kwa watumiaji wenye vifaa vya Android tuu na pia ukiona umeshindwa au umekwama katika kutumia njia moja basi huna budi kujaribu na njia nyingine.
Endelea kufurahia WhatsApp yako! Pia kama ungependa TeknoKona iandike kuhusu kitu fulani basi unaweza kutuandikia sehemu ya comment au katika mitandao yetu ya kijamii na sisi tutafanya hivyo
One Comment
Comments are closed.