fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple Galaxy IPhone Samsung simu Smartphones

iPhone Ya Kujikunja Yazidi Kununukia, Teknolojia Ya Galaxy Z Fold 3 Yahusika!

iPhone Ya Kujikunja Yazidi Kununukia, Teknolojia Ya Galaxy Z Fold 3 Yahusika!

Spread the love

Sasa hivi simu janja za kujikunja ni nyingi mno na kwa sasa teknolojia hii kwa kiasi kikubwa imeanza kuzoeleka.

Tumeshaandika sana kuhusu simu na vifaa mbali mbali vinavyotumia teknolojia ya kujikunja HAPA, pitia kwanza kidogo.

Mfano Usio Halisia Wa Simu Ya iPhone Ya Kujikunja 2

Mfano Usio Halisia Wa Simu Ya iPhone Ya Kujikunja 1

Taarifa zilizopo ni kwamba Kampuni ya Apple inatumia teknolojia ya OLED ambayo imetumiaka katika Samsung Galaxt Z Fold 3 ambayo inasemekana ndio teknolojia kubwa katika simu za kujikunja kwa sasa.

Hii inaonekana ni hatua moja wapo katika kuhakikisha kuwa kampuni inatengeneza iPhone, iPad, au hata Mac ya kujikunja (lakini jicho letu kwa sasa lipo kwenye iPhone).

K

Mfano Usio Halisia Wa Simu Ya iPhone Ya Kujikunja 4

Mfano Usio Halisia Wa Simu Ya iPhone Ya Kujikunja 2

umbuka kitu kimojawapo kinachofanya teknolojia hii makampuni mengi kushindwa ni kwamba ni vigumu sana kufanya kioo kikawa na wembamba unaotakiwa kuweza kujikunja hata kwa miaka kadhaa mbeleni.

SOMA PIA  Kuwa Tayari Kwa Emoji Mpya Na Nzuri Zaidi!

Teknolojia ambayo Samsung wameitumia katika Samsung Z Fold 3 mpaka sasa  imeonekana ikifanya vizuri tuu na pengine ndio sababu husika Apple nao wakaona wasibakie nyuma.

Mfano Usio Halisia Wa Simu Ya iPhone Ya Kujikunja 3

Mfano Usio Halisia Wa Simu Ya iPhone Ya Kujikunja 3

Mpaka sasa hizi ni taarifa tuu ambazo zipo na haijulikani muda ambao Apple watazalisha kifaa kutoka kwao ambacho kinajikunja ambacho pia kitatumia teknolojia hii.

SOMA PIA  Punguzo la bei ya betri kwa simu za iPhone

Ila nikuahidi tuu kikijulikana hatutosita kukujuza, ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika uwanja wa comment, hili umelipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania