Wengi tunapenda kutumia kompyuta kuangalia movie na series, kusikiliza muziki au kuelekeza mada mikutanoni na darasani. Shida inakuja pale tunapoanza kuzunguka huku na kule na inatubidi kurudi tena kwenye kompyuta kuiamuru kucheza nyimbo mpya au kusukuma kurasa. Adha hii inachosha ila kuna suluhisho.
Habari nzuri ni kuwa inaweza kupunguzwa kwa kutumia simu yako ya mkononi. Ndio, inawezekana kabisa kutumia simu-janja kuamuru kompyuta yako kufanya jambo utakalo kama vile unavyotumia rimoti kuamuru luninga. Kuna programu kadhaa zinazokupa uwezo wa kufanya hivyo ikiwemo programu ya ‘Unified Remote’ ambayo inapatikana kwa simu zenye mfumo wa Android, Windows na simu za I-phone.
Kwa mifumo ya Android, Unified Remote inapatikana kwenye playstore au unaweza kuipakua kwenye tovuti ya www.unifiedremote.com/. Kwa kutumia programu hii unauweza kuamuru programu kama Windows Media Player na VLC kucheza nyimbo au ‘episode’ mpya. Kwenye mikutano, unaweza kuitumia kusukuma kurasa kwenye skrini ya projekta au kuelekeza mambo muhimu kwa kutumia mshale na hata kuandika kitu bila kusogelea .
Baada ya kuipakua kwenye playstore na tovuti, hakikisha umeipakia Unified Remote kwenye simu yako na kwenye kompyuta yako ili simu iweze kuwasiliana na kompyuta. Kuanza kuamuru kompyuta kufanya mambo mbalimbali, kwanza unganisha simu yako na kompyuta kwa kutumia ‘wireless hotspot’, huduma ambayo inayopatikana kwenye simu yako ya android. Kisha washa Unified Remote kwenye kompyuta na pia kwenye simu. Sasa, unaweza kutumia simu yako kuamuru kompyuta yako.
No Comment! Be the first one.