Niliandikia kuhisiana na jukwa ala Gmail kupata muonekano mapya >>HAPA<< na kwa sasa hali imebadilika imekua sio kama mwanzo.
Mwanzoni ni kwamba –ndani ya Gmail– ulikua na uwezo wa kuhama kutoka katika toleo moja hadi linguine (la nyuma na la mbele) pale unapojisikia tuu lakini kwa sasa hali sio kama zamani.
Google wao wanasema walitoa toleo hili jipya ikiwa ni moja ya njia ya kuahakikisha kuwa huduma nyingi za Google zinapatikana katika eneo moja.
Kingine cha msingi ni kwamba toleo hili jipya ndani ya mwezi huu litaanza kupatikana kwa watu wote duniani bila kusahau kuwa haitawezekana tena kurudi katika toleo la nyuma.
Kwa wale ambao tushaanza kutumia toleo hili sidhani kama tuna cha kujutia? Huduma kama Chat, Spaces, na Meet vyote tunavipata sehemu moja.
Kingine ni kwamba hata kwa wakati ambapo ulikua unaweza kurudi katika toleo la nyuma bado mtandao wa Google uliweka wazi kuwa kuna muda ukifika hilo halitawezekana tena.
Wazi ni kwamba, huo wakati ndio mwezi huo, japokua mtandao huo haujaweka wazi kuwa ni tarehe gani ambayo wamepanga kufanya jambo hili.
Kwa haraka haraka kuna urahisi sana wa kutumia toleo hili jipya kuliko la zamani maana kila kitu unakikuta katika upande wa kushoto ili kukipata kwa uharaka kabisa.
Vile vile unaweza ukaamua kutumia Themes ili kubadilisha muonekano wa Gmail kwenda katika ule unaoutaka wewe. Ni wazi kuwa Gmail ndio jukwaa la kutuma na kupokea barua pepe linalopendwa sana na watu na pia ndio jukwaa lenyewe watumiaji wengi sana.
Ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unaendelea kutumia toleo la zamani la Gmail? Au umeshaanza kutumia toleo jipya?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.