Kipengele hiki hakikuwepo kabisa katika mtandao wa Instagram na ilikua kama ukitaka kuliwezesha hili ni lazima uwe na App nyingine – sasa litawezekana kwa baadhi ya akaunti katika mtandao huo.
Instagram ni mtandao wa kijamii ambao unatumiwa na watu wa aina tofauti tofauti na hata hivyo kila mtu ana lengo la kutumia mtandao huo sio?
Mambo ni mengi, pengine kuna wengine wanashindwa pata muda muafaka wa kuingia na kutuma kitu katika mtandao huo – sababu kama vile ukosefu wa intanet, kuwa bize nk zinaweza kuwa ni sababu – lakini wa kupitia kipengele hichi hali itakua shwari.
Ufanyaji kazi wa kipengele hiki ni kwamba unaweza ukaamua kupangilia post zako muda wake wa kuji’post katika mtandao huo –mfano unaweza ingia katika mtandao na ukaamua post yako iruke baada ya siku mbili lakini ukawa tayari umeitayarisha iwe hivyo.
Kingine ni kwamba watakao furahia huduma hii sio wote, hii ni kwa zile akaunti ambazo ni za mfumo ule wa wafanya biashara na wazalishaji wa maudhui (ni lazima uwe umeseti akaunti yako hivyo).
Kipenge hichi kinaweza kusaidia watu kuweza kupanga ratibu ya kuruka kwa Picha/Video au hata Reel hadi siku 75 kabla kwa kutumia App ya istagram.
Kipengele hiki kilikua katika majaribio katika kipindi cha miezi ya nyuma, kwa sasa kina watu kadhaa tuu ambao wanaweza kukikutumia.
Japokua haiku wazi ni lini kitaanza kutumika kwa watumiaji wote lakini inabidi watumiaji wengine wa mtandao wa instagram kusubiri kipengele hichi mpaka kitakapo wasili kwao.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je wewe umeshaanza kukitumia kipengele hiki? Kama bado je una shauku ya kuanza kukitumia?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.