Kampuni ya TALA inayokopesha kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi, imetangaza kufunga shughuli zake Tanzania.
Imetoa taarifa hiyo Jumanne Septemba 17, 2019 na kubainisha kuwa maelezo ya kina kuhusu uamuzi huo yatatolewa hivi karibuni.
Kampuni hiyo inayoendeshwa na teknolojia ambayo kwa sasa inafanya kazi nchini Kenya, Mexico,
India na Ufilipino hutoa mikopo ya haraka, na binafsi kwa wakopaji na kuvutia zaidi ya watu milioni 27 duniani.
“Tunasikitika kukutaarifu ya kwamba Tala kwa sasa haitatoa mikopo Tanzania. Tunashukuru kwa kutupa nafasi ya kukuhudumia na kuwatakia wateja wetu mafanikio.Wateja ambao bado wanadaiwa wanaweza kulipa mikopo yao. Tumia Tigo-Pesa lipa namba 888000 and nambari ya simu uliojisajilia na Tala kama akaunti yako,” inasomeka taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo.