fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook Ndege Teknolojia

Ndege ya huduma ya intaneti kutoka Facebook yapata ajali ktk majaribio

Ndege ya huduma ya intaneti kutoka Facebook yapata ajali ktk majaribio

Spread the love

Kampuni ya Facebook imekuwa imejikita katika utengenezaji wa ndege ndogo zinazotumia umeme wa jua zitakazokuwa na uwezo wa kurusha huduma ya intaneti kwa mamilioni ya watu watakuwa eneo ambalo ndege hizo zitakuwa zinaruka.

Ndege ilifanikiwa kuwa hewani kwa takribani dakika 90, ila ilipata hitilafu na kuanguka wakati ikijaribu kutua. Ndege hizi ndogo zinatumia umeme wa jua kupaa na kurusha huduma ya intaneti kwa eneo la chini – hii italenga sehemu zinazokosa huduma hiyo au huduma hiyo inapatikana kwa shida.

SOMA PIA  Ripoti: Biashara ya mtandaoni yaongezeka kwa wananchi wa Kenya

watoto facebook

 

Majaribio ya ndege hiyo iliyopewa jina la Aquila yalifanyika mwezi Juni tarehe 28 mwaka huu.
Ndege hiyo ilifanikiwa kupaa bila shida yeyote, waandisi wa kampuni hiyo walifanikiwa kusoma data mbalimbali zinazohusu majaribio hayo wakati ndege hiyo ikiwa angani – tatizo pekee lilitokea pale tuu ndege ilipokuwa inatua.

Mpango mzima ulikuwa kufanya majaribio hayo kwa muda wa dakika 30 ila baada ya ndege hiyo kuwa angani ulifanyika uamuzi wa kuiweka ndege hiyo angani kwa muda mrefu zaidi.

Tatizo lilitokeaje?

huduma ya intaneti kutoka Facebook

Ubawa wa ndege ya huduma ya intaneti kutoka Facebook, mbawa zake zitakuwa na ‘cells’ kwa ajili ya kutengeneza umeme wa jua

Eneo la majaribio ni eneo la jangwa na kila muda ulivyokuwa unazidi kwenda ndio anga likawa na joto zaidi na upepo mkali. Vitu hivi vilichanganya mfumo wa kompyuta wa kuindesha yenyewe ndege hiyo na hivyo makosa ya kimaesabu yalisababisha ndege hiyo iende kwa kasi zaidi kitu kilichasababisha bawa lake moja kuharibika na hivyo kuiangusha vibaya ndege hiyo wakati inajitahidi kutua.

SOMA PIA  Baada ya Huawei Mate 10 kutoka sasa ni zamu ya Huawei Mate 10 Pro

Nini wamejifunza Facebook?

Wenyewe wamesema lengo lao la kujifunza zaidi limekamilika. Lengo lao kwa ndege hizo ni kuruka na kutumika mara moja tuu. Kikubwa ni kwamba ilifanikiwa kupaa vizuri na kukaa angani na kufanya kazi kama malengo yao yalivyo, wataona vitu vya kuboresha na tutegemee kusikia maendeleo zaidi kwenye mpango wao huu.

SOMA PIA  Roketi ya V2 - Roketi ya Vita vya pili vya Dunia iliyojenga teknolojia ya safari za anga

Huduma ya intaneti kutoka Facebook  inakuja. Suala ni ‘LINI’ – tunategemea kwa kiasi wanachowekeza katika teknolojia hii basi hadi kufikia mwaka 2018 kuna uwezekano mkubwa tukaona wakaanza kutoa huduma hiyo.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania