fbpx
Diski, Kompyuta, Teknolojia, Windows

Je kwa nini diski zinaanza na namba C badala ya A? #Windows

diski-zinaanza-na-namba-c-badala-ya-a-windows
Sambaza

Je ushawahi kujiuliza kwa nini diski zinaanza na namba C badala ya A kwenye kompyuta zinazotumia Windows? Leo fahamu.

Kwa watumiaji wa kompyuta wa tokea miaka ya 90 ni rahisi wao kuelewa sababu, au kutojua sababu ila washawahi kutumia kompyuta wakati diski zinatambulika pia kwa namba A.

Historia

  • Programu endeshaji ya Windows ilitengenezwa juu ya mfumo endeshaji mwingine wa kwanza kutoka Microsoft uliokuwa unatambulika kwa jina la MS-DOS. Kipindi hicho mfumo wa diski za flopi ndio zilikuwa zinatumika (floppy drives).

    diski za flopi Je kwa nini diski zinaanza na namba C badala ya A?
    Je kwa nini diski zinaanza na namba C badala ya A?: Muonekano wa diski za Flopi
  • Katika kompyuta hizo kompyuta ilikuwa ina uwezo wa kutumia hadi diski za flopi mbili kwa wakati mmoja na hivyo moja kwa moja ya kwanza ilichukua nafasi ya utambulisho wa A: na ya pili ikachukua nafasi ya utambulisho wa B:.

Baadae diski za mfumo wa ‘harddrives’ zilivyokuja ndio zikachukua nafasi ya C:, na mgawanyo wa diski (partition) wa pili au diski nyingine ndani yake ndio ikachukua nafasi ya D:, sehemu ya cd, yaani CD-ROM ndio ikapewa nafasi ya E:

Hiyo ndio historia fupi na sababu kuu kwa nini diski kwenye kompyuta yako kwa sasa zinaanza na kubeba namba C:, ila kumbuka teknolojia ya utambuzi wa diski za flopi bado upo kwenye Windows. Mfano ukiwa na kimashine cha kutumia flopi na ukakipachika kwenye kompyuta yako basi flopi itatambulika kwenye Windows na itachukua namba A:

flopi diski floppy disk kwenye windows kompyuta
Diski ya Floppy ikitambulika kwenye kompyuta ya Windows 7

Je ni jambo gani jingine la kiteknolojia unalolitumia na ungependa kufahamu historia yake? Tuambie kwenye komenti. 🙂 Fahamu na Jifunze mengi kuhusu kompyuta hapa -> Teknokona/Kompyuta

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Muonekano wa giza unapunguza matumizi ya betri
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |