Licha ya kampuni kuwa ni kubwa sana na lenye faida kupindukia lakini bado halilali. Apple kila siku wanahakikisha kuwa wanaboresha na kurahisisha mawasiliano baina ya watu kwa kutumia simu zake.
Kutokana kwamba watumiaji wa iPhone wanaongezeka kwa kiasi kikubwa hivyo kampuni la Apple limejikita katika kuhakikisha kuwa watumaiji wake wanaweza fikia na kuanza kutumia vifaa hivyo kwa urahisi kabisa. Hii ikijumuisha na jinsi ya kuweka teknolojia ya utambuzi wa alama za vidole (finger print)
Katika mkutano ambao ulifanyika Aprili 15, kampuni liliweka wazi juu ya jinsi watu wanvyotumia simu zao kwa siku na kampuni ikakiri kuwa ni vyema kulinda kila kitu wanachofanya katika simu hizo.
Licha ya hayo yote kampuni ilisema kuwa mtu wa kawaida huwa anatoa loki ya simu yake ya iPhone mara 80 kwa siku. Hii inamaanisha kuwa wamiliki wa simu za iPhone huwa wanatoa loki za simu zao mara 6 au 7 kwa kila lisaa. Au kwa haraka haraka mwingine anaweza akasema mara moja kila baada ya dakika kumi na hiyo ni kama mtumiaji atatumia simu hiyo kwa masaa 12.
Taarifa hii imetolewa na kampuni la Apple baada ya maboresho katika ulinzi na usalama wa simu hizo. Kampuni linasema tangia lilipoweka uwezo wa mtu kuweza kutoa loki ya simu kwa kutumia alama ya vidole, idadi ya kungalia simu kwa siku imeongezeka
Hii ni tofauti na jinsi ilivyokuwa mwanzo wakati mtu ili kutoa loki ilibidi aweke neno siri. Android wao walisemaga kuwa simu zao zinatolewa loki na mtu wa kawaida mara 110 kwa siku. Lakini kumbuka namba hizi za utoaji loki zinaweza zikatofautia baina ya mtu na mtu
Mpaka sasa kampuni imepiga hatua kubwa katika swala zima la kuingiza neno siri kwa kutumia alama za vidole lakini kumbuka kuna baadhi ya maeneo bado kampuni inabidi liendelee kuumiza kichwa ili kuweka ulinzi mkubwa na wa usalama. Mfano katika iCloud kampuni inabidi ipaangalie kwa jicho la tatu (japokuwa nadhani wanapaangalia kwa jicho la nne)