fbpx

Apple, apps

AppStore: Apple yaondoa VPN kwa simu za iPhone nchini China

apps-za-vpn-kwa-simu-za-iphone-nchini-china

Sambaza

Ripoti kadhaa zilizojitokeza mwishoni mwa wiki zimedai kuwa kampuni ya Apple imeondoa apps za VPN katika AppStore  kwa watumiaji wake nchini China.

Watengenezaji wa apps hizo ikiwemo wa StarVPN, VyprVPN na ExpressVPN walisema siku ya jumamosi kwamba apps zao zimeondolewa kutoka kwenye App Store.

Kuondolewa kwa apps/programu za VPN kunadaiwa kwamba ni kinyume na sheria za China hivyo kampuni ya Apple imelazimika kuziondosha programu hizo ambazo ni kinyume na taratibu za nchi ya China.

INAYOHUSIANA  WhatsApp waja na aina mpya ya Muandiko (font style)

VPN hutumiwa na wananchi wa China ili kuweza kutumia mitandao ambayo kwa nchini China imezuiwa kuonekana kama Google, Facebook, Pinterest, New York Times, Dropbox na mengineyo kadhaa.

Mapema mwaka huu Wizara ya Viwanda na mambo ya Teknolojia ya habari ilitoa taarifa kwamba watengenezaji wote wa VPN wanapaswa kupata leseni kutoka serikalini.

Rais wa kampuni inayotengeneza VyprVPN alisema amesikitishwa na kampuni ya Apple kuondoa programu za VPN kwa shinikizo la serikali ya China hata bila ya kutaja sheria au kanuni ambayo inaifanya VPN kutokuwa halali.

INAYOHUSIANA  Matangazo kwenye simu: Jinsi ya kuzuia matangazo kwenye simu za Android

Aidha ameishutumu kampuni ya Apple kwa kuisaidia serikali ya China katika juhudi za kudhibiti mitandao ya nje ambao ni kinyume na haki za binadamu.

Serikali ya China imekuwa ikidhibiti mitandao ya kutoka nje ya nchini hiyo katika kile inachodai ni kulinda na kuenzi tamadamu zake kutokuathiriwa na mitandao ya nje.

Vipi wewe una mtazamo gani juu ya maamuzi haya?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.