Mtandao wa kijamii wa Facebook kuja na app ya kamera ili kusaidia kuwafanya watu wapost picha nyingi zaidi kwenye mtandao huo.
Data za mtandao huo zinaonesha watumiaji wa mtandao huo siku hizi hawapost picha na maneno (status) kwa wingi ukilinganisha na zamani.
Suala la watu kuwa katika mtandao wa kijamii na kutokupost mambo linaonekana ni jambo hatari sana kwani litafanya watu wasiwe wanazungumza sana na mwishowe wengi wataboreka na mtandao huo na hivyo kuacha kuutumia. Inasemekana suala hili ni moja ya sababu ya kufa kwa mitandao mingine mikubwa zamani kama vile MySpace.
App hiyo inayoonekana kuiga muonekano na jinsi vile app ya Snapchat inavyofanya kazi katika upigaji picha – inategemewa itawawezesha watumiaji wake kupost picha na video kwa haraka zaidi kwenda kwenye akaunti zao za Facebook ukilinganisha na hali ilivyo sasa.
Data zinaonesha asilimia 37 tuu ya watumiaji wa mtandao huo walipost picha katika kipindi cha mwezi wa 7 hadi wa 9 mwaka 2015, hili lilionesha kupungua kwani katika kipindi kama hiko kwa mwaka 2014 ni asilimia 59 ya watumiaji wake walipost picha katika mtandao huo.
Mtandao wa Snapchat unaonekana ndio wenye ukuaji mkubwa sana katika eneo la post za picha katika mitandao ya kijamii. Facebook tayari walijaribu kuleta apps za kushindana na Snapchat kupitia app yao ya Slingshot iliyoletwa Disemba 2014 na pia kupitia app ya Poke – lakini zote zilishindwa kufanya vizuri.
App hiyo ina nafasi ya kufanikiwa kama itawezesha uwezo wa kurusha video za LIVE kwenda kwenye mtandao huo….ingawa hili linaonekana litawavutia watu wachache tuu hasa hasa katika nchi zilizoendelea.
Waandishi nguli wa mitandao kama ya The Forbes na The Verge wanaona ata app hii itakuwa na mwisho mbaya. Inasemekana Facebook imepoteza mvuto mkubwa kwa vijana katika suala la kutuma posts za picha n.k kwani ukuaji wa Facebook umemaanisha ni rahisi kujikuta ukiwa na urafiki na ndugu wa karibu au mabosi wa kazini na hivyo vijana wengi wamekuwa wagumu kutuma post kwa wingi ukilinganisha na zamani.
Je wewe unadhani unaitaji app ya kamera kutoka Facebook kwa ajili ya kupostia picha na video kwenye profile yako? Au ni kitu kisicho na ulazima?
Vyanzo: TheVerge, The Forbes na mitandao mbalimbali