Kile kilichokuwa kinazungumziwa kwa muda mrefu kinaonekana sasa kipo njiani kutokea rasmi. Apps za Android kuweza kutumika katika kompyuta zinazotumia programu endeshaji ya Chrome OS.
Kwa muda mrefu vyanzo mbalimbali vilisema kuna uwezekano mkubwa wa programu endeshaji ya Chrome OS kutoka Google kupata uwezo wa kutumia apps za Android moja kwa moja bila mtumiaji kufanya chochote.
Tulishaandika kabla kuhusu uwezekano wa hili hapo mwaka jana – Android na Chrome OSÂ kuunganishwa. Hatua hii inaleta uwezekano mkubwa wa programu endeshaji hizi mbili kuwa moja.
Kwa sasa njia pekee ya kumuwezesha mtu kupakua apps za Android katika Chrome OS ilikuwa ni kwa kutumia njia ngumu wanayoweza fanya watu waliokubuhu katika masuala ya kompyuta(developers). Hili liliweza fanikiwa kupitia project inayotambulika kwa jina la App Runtime for Chrome (ARC)
Kuna watumiaji wa Chrome OS ambao wamekutana na chaguo linalotokezea kama ‘pop up’ pale wanapoingia eneo la settings linalowapa chaguo la kukubali kutumia Google Playstore kwenye kompyuta zao. Ila kabla hawajachagua chaguo hilo ujificha.
Inaonekana ni kitu ambacho tayari kipo kwenye matengenezo na Google wanaweza kukileta rasmi kwenye matoleo (UPDATES) mapya ya Chrome OS.
Developers kadhaa walifanikiwa kupitia code za ndani za Chrome OS na kweli wakakutana na code zinazoonesha uwezo huo.
Watu wengi wanaona uwezo huu utazidi kukuza mafanikio kwa programu endeshaji ya Chrome OS kutokana na apps nyingi zinazopatikana katika soko la Google Play ukilinganisha na zile za Chrome zinazopatikana katika soko la apps la Chrome Web Store.
Programu endeshaji ya Chrome OS kwa sasa hairuhusu app yeyote ya kivinjari kingine na wengi wanaona ujio wa Google Playstore utaweza wezesha kwa mara ya kwanza watumiaji wa programu endeshaji hiyo kutumia hadi vivinjari vingine… Je itawezekana? Endelea kutembelea TeknoKona!