Makampuni mengi yanyojihusisha na teknolojia siku hizi yanathamini ulinzi na usalama wa taarifa za wateja wake sana. Kwa mfano tumeona kampuni la Apple likipinga maamuzi ya FBI kutaka kufungua moja ya simu yake (iPhone)
Sawa pengine baada ya tukio hilo la iPhone ndio limepelekea mtandao wa WhatsApp kuimarisha ulinzi wa mazungumzo baina ya mtu na mtu (End-To-End Encryption).
Njia hii ya ulinzi na usalama ina uwezo mkubwa wa kuzuia serikali, wadukuzi na watu wengine kuweza kupekua kwa siri taarifa zako za mazungumzo baina yako na mtu mwingine. Kumbuka awali ilikuwa ni rahisi kabisa kujua watu wanazungumza nini katika mitandao yao ya kijamii kwa kuwa teknolojia hii ilikuwa haijaanza tumika sana
Sasa Viber nao wameamka na kusema “Hapana Hatuwezi kubaki nyuma” katika teknolojia hii. Kama ilivyo katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp. Huduma hii ya ulinzi na usalama itakuwezesha kutuma na kupokea mazungumzo ambayo yana ulinzi wa hali ya juu kabisa.
End-To-End Encryption inapatikana katika toleo la Viber namba 6.0. Kingine kizuri kuhusiana na teknolojia hii ni kwamba hata mtandao wenyewe utakuwa hauna uwezo wa kusoma meseji zako. Yaani kwa mfano ukiwa unatumia teknolojia hii mitandao kama vile VIber na WhatsApp itashindwa soma meseji zinazoenea kupitia mitandao yake.
Wakati unafanya mazungumzo na mtu utaona kimetokea kikufuli chekundu, ukiona hivyo tuu basi jua inamaanisha kwamba mazungumzo yenu yanalindwa
Viber imesema kuwa Toleo hili mpaka kufikia muda wa siku mbili litakuwa tayari linapatikana duniani kote. Viber ina watumiaji zaidi ya milioni 700 ambao wanatumia mtandao huo mara kwa mara. Na kwa maboresho haya namba hiyo inaweza ikapanda kwa sababu watu wanapenda usalama
Apple ndio lilikuwa kampuni la kwanza kuja na teknolojia hii na ikafuatiwa na WhatsApp na sasa Viber. Inaonekana kabisa makampuni haya matatu yanajali sana taarifa za watumiaji wake. Lakini tusubiri tuone maana tunaweza tukashangaa makampuni mengine mengi yakajiunga na teknolojia hii