Kuna uvumi umesambaa mitandaoni kwamba mtandao maarufu wa Snapchat unajipanga kutengeneza miwani janja kama zile za Google glass. Teknolojia hii mpya inategemewa kuwaruhusu watumiaji wa Snapchat kuweza kuona snaps za marafiki zao kupitia miwani.
Tetesi hizi zimepewa nguvu na taarifa za Snapchat kuwaajiri wataalamu mbalimbali ambao ama wanautaalamu wa mambo ya miwani janja ama wamekwisha fanya kazi katika makampuni yanayojishughurisha na utengenezaji wa miwani janja.
Snapchat inaye msanifu wa vifaa vya macho anayejulikana kwa jina la Lauryn Morris ambaye alikwisha wahi kufanya kazi katika kampuni maarufu ya Michael Kors, pia mtandao huu umemwajiri Mark Dixon ambaye alifanya kazi na Microsoft katika project yao ya Halolens.
Snapchat wanaonekana kujaribu kukwepa kitu ambacho kimekuwa kikiikumba mitandao mingi ambayo hupata umaarufu lakini hufa muda mchache kutokana na kutokuwa na kushindwa kukuwa kiuchumi. Miwani janja ni njia bora ya kuufanya mtandao huu kuwa zaidi ya mtandao wa kawaida, mauzo ya miwani hizi kwamfano yataifanya Snapchat kuongeza thamani yake katika soko na kukwepa mambo ambayo yanawakuta Twitter kwa mfano.
Ingawa Snapchat wenyewe hawajasema chochote juu ya tetesi hizi, ikumbukwe kwamba mwaka jana kulikuwa na tetesi za kuundwa kikosi kazi ndani ya Snapchat ambacho moja ya majukumu yake ilikua ni kuhakikisha kuangalia upya ni aina gani ya vitu watumiaji wao wanavitazama zaidi. Hii inaleta picha kwamba mtandao huu ulikuwa wanachunguza ni kwa namna gani wanaweza kuiendeleza huduma yao na bila shaka jibu tunalo sasa.
Ingawa hii ni habari nzuri lakini kwa makabwela ama watumiaji wa kipato cha chini na cha kati huu ni msumari unpigiliwa katika kidonda kwa sababu miwani janja hizi hazitakuaja kwa bure. Kwa mfano Miwani janja ya google (Google glass) ni shilingi za kitanzania 3,276,750 (KSh 152,315.25 ) japokuwa bei ya miwani janja hizo za Snapchat bado lakini lazima zitakuwa zinakaribiana na bei za Google glass. Hivyo pengine watumiaji wa kawaida wa Snapchat wataishia kuona tu na wasiweze kununua miwani hizo.
Endelea kutembelea mtandao wako wa teknokona nasi tutakuhabarisha jambo lolote linapotokea tena katika lugha yetu adhimu ya Kiswahili
Vyanzo: Techcrunch na mitandao mbalimbali