Kama utakuwa ni mtu ambae unatumia Instagram hasa vikatuni (emoji) mabalimbali pale unapoandika kitu kwenye mtandao huo wa kijamii utakuwa umebaini ni kwa namna gani hivi sasa ilivyokuwa rahisi kutumia vitu hivyo.
Sasa hakuna haja ya kufungua sehemu ya kutoa maoni ili kuweza kutumia kikatuni bali vimesogezwa kwenye uso wa mbele (chini kidogo ya pale ambapo maelezo ya kile kilichochapishwa).
Instagram wameamua kuweka karibu kabisa zile katuni zinazopendwa kutumiwa na idadi kubwa ya watu.
Maboresho hayo yanapatikana programu endeshi maarufu; Android na iOS. Suala hilo haimaanishi kuwa vikatuni vingine vimeondolewa, la hasha! Bali zile ambazo zinapendwa ndio zimesogezwa karibu.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
3 Comments
Comments are closed.