Snapchat walikua na kipengele kinachowawezesha watu kuweza kujua nani marafiki zao wa karibu yaani “Best Friends”. Kwa sasa hicho kiioengele kimeachwa na kuanzishwa kipengele kipya ambacho kinajikita zaidi katika Emoji.
Kipengele hiki kipya kina usiri zaidi kuliko kile cha mwanzo na hakita toa sura kama ile ya mwanzo kwa watumiaji wake.Kipengele hiki kilitolewa na blog katika mtandao wa snapchat katika kipengele cha discovery.
Blog hiyo ilisema watu wategemee emoji katika list ya marafiki zao katika mtandao huo wa snapchat.Kipengele hiki kinaweza kuonyesha wakina nani ni marafiki wa karibu na nani ni rafiki wa karibu wa nani. Hili litafanyika bila kuonyesha majina (user name) yao kwa watu wengine kama mwanzo ilivyokuwa. Yote haya yatafanyika kwani pale katika list ya majina ni emoji tuu zitakua zinatokea.
Emoji tofauti tofauti zinawakilisha mambo tofauti tofauti, kwa mfano emoji ya moyo wa dhahabu hii ikiwa katika rafiki yako itamaanisha kuwa ndio rafiki yako wa karibu wa kwanza (1) au mtu ambae mnatumiana sana snap na anakutumia sana snap.
Emoji ya sura ya furaha ina maanisha kuwa mtu huyo ni moja kati ya marafiki zako wa karibu au huwa unatumiana nae snap mara kwa mara. Miwani inamaanisha una ‘share’ rafiki na mtu mwingine. Tabasamu la kejeli litamaanisha kuwa ni rafiki yako wa karibu lakini yeye hakuchukulii kama rafiki wa karibu.
Emoji ya moto inamaanisha kuwa wewe na huyo mtu mlikua mnatumiana snap sanaaaaa kipindi cha nyua lakini sasa kila mtu ana mtegemea mwenzie.
Snapchat inaonekana kujitahidi katika kipindi cha mda mchache tu. Vipengele vingi vimeongezwa na kampuni hilo katika mtanndao wake huo wa kijamii. Moja katika ya hatua iliyofanywa na snapchat ni kile kipengele cha Discovery ambacho makampuni ya habari yanaweza tangaza habai zake. Discovery ni kama uwanja wa matangazo lakini ni matangazo ambayo mtumiaji anaweza kuchagua kuya angalia au kuto angalia.
Kujua zaidi kuhusu Emoji zingine bofya hapa
Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram
No Comment! Be the first one.