fbpx
Gari, Magari, Teknolojia

Toyota na Suzuki kuunganisha nguvu katika teknolojia za magari

toyota-na-suzuki-kuunganisha-nguvu-katika-teknolojia-za-magari
Sambaza

Makampuni ya Toyota na Suzuki ya nchini Japani yakubaliana kuwa na uhusiano katika masuala ya teknolojia za magari.

Toyota na Suzuki yanashindana lakini Suzuki imejikita zaidi katika utengenezaji na uuzaji wa magari yenye maumbo madogo.

 

toyota na suzuki

Wametangaza leo wakisema uhusiano wao utahusisha maeneo ya teknolojia rafiki wa mazingira, usalama na teknolojia nyingine zinazohusiana (kama information networking).

Katika makubaliano haya ni Suzuki itakayonufaika zaidi hasa hasa ukilinganisha kitu kama bajeti ya masuala ya utafiti -ambapo Toyota ana nguvu zaidi kipesa. Ila pia Suzuki ni bingwa katika utumiaji wa teknolojia nafuu na utengenezaji wa magari madogo na rafiki wa mazingira zaidi.

Rais wa Toyota

Rais wa kampuni ya Toyota Motor Corp. Bwana Akio Toyoda amesema kwa hali ya soko ya sasa hivi ni kupitia kushirikiana tuu ndio kampuni zinaweza kudumu na kufanya vizuri.

Mwenyekiti wa kampuni ya Suzuki Motor Corp. Bwana Osamu Suzuki amesema amekuwa akisubiria kwa hamu makabaliano hayo, na akasema alishawahi kumwambia baba yake Toyoda muda mrefu uliopita kuhusu kuwa na ushirikiano. Baba yake Rais wa Toyota anashikilia nafasi ya uenyekiti wa kampuni ya Toyota, anaitwa Shoichiro Toyoda.

Toyota tayari imejikita vizuri katika masuala ya teknolojia za magari ya kujiendesha yenyewe na pia kwenye teknolojia ya magari ya umeme. Ushirikiano huu unaweza kuwasaidia wote wawili katika maeneo haya na mengine mengi.

Vipi una mtazamo gani juu ya ushirikiano huu? Tuambie kwenye comment, tunafurahi kusikia kutoka kwako.

Vyanzo: SFGate na tovuti mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Uwezo wa watu wanne au zaidi kuweza kuwasiliana kupitia WhatsApp
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |