Tangia taarifa zitoke ambazo zilishangaza wengi kwamba mtandao wa Vine ambao unamilikiwa na Twitter kwamba hautoweza kuendelea kwa sababu Twitter wanaachana nao
Wengi walijitolea kuusaidia mtandao huo kutokana na lile ambalo twitter walisema. Baadhi ya watu hao ilikuwemo pamoja na watu wenye majina makubwa katika mtandao huo lakini jitihada zikagonga mwamba.

Ukiachana na mtandao huu kufikia tamati (kifo) waanzilishi wake wawili walipanda gari lingine na kuamua moja kwa moja kuzalisha mtandao mwingine ambao unahusisha maswala ya video.
Katika mitandao ya kijamii kwa sasa watu wanapenda sana kuangalia video kuliko hata kusoma maelezo marefu ambayo mara nyingine yanakuwa yameambatana na picha.

Mtandao huu mpya wameupa jina la ‘Hype’ na utakuwa ni ule wa zile video za ku’stream’ na kwa sasa mtandao huo unapatikana katika toleo la majaribio (beta) kwa watumizi wa iOS tuu,
Waanzilishi hao (Bw. Rus Yusupov na Colin Kroll) kama inavyojulikana wana historia nzuri juu yao kwani vichwa hivyo viwili vinavyokutanaga huwa jambo zuri linatokea. Ila hata hivyo kwa upande mwingine ni kwamba inakua ni vigumu sana kuliteka soko la video kwa sasa ambalo tayari limeshatawalwa na makampuni makubwa kama vile Facebook Live.

Cha kufurahisha ni kwamba hata hizo video zako za Hype unaweza ukazisambaza katika mtandao wako wa kijamii wa Twitter. Hii inaonyesha kuwa bado waanzilishi hawa wana mahusiano mazuri na twitter au wanataka kuipiku huduma ya Twitter ijulikanayo kama periscope.
Ukitaka kuona jinsi mtandao huu ulivyo ingia katika soko ukiwa na simu yako ya iOs na vile vile kwa watumiaji wa Android hivi karibuni mzigo utashuka katika vifaa vyenu