Samsung imekuwa imekuwa ikitoa masasisho kwenda kwenye simu janja zake kwa miaka mingi tuu lakini katika siku za karibuni kampuni hiyo imeongeza kasi ya kuzifikia rununu nyingi zaidi ndani ya kipindi kifupi.
Wengi wetu tutakuwa na taarifa kuhusiana na tatizo ambalo lilibanika kwenye vipuri vya Qualcomm wiki chache zilizopita jambo ambalo limefanya kampuni ambazo simu janja zao zinatumia kifaa hicho cha mawasiliani kuangalia namna ambavyo rununu za wateja wao zinabaki kuwa salama.
Samsung imejitahidi inapeleka masasisho ya mwezi Mei 2021 kwenye rununu nyingi zaidi hivyo kuongeza idadi ya simu janja ambazo zimeshafikiwa na maboresho hayo. Tukiwa mwanzoni mwa wiki Samsung wamezitaja simu ambazo zinatarajiwa kupokea/tayari zimeshapokea masasisho hayo muhimu hasa ukizingatia na hili lililobainika kuhusu vipuri vya Qualcomm. Simu janja hizo ni:
Simu za Galaxy A
Simu janja zilizo chini ya familia hii ni:-
- Galaxy A12 — A125FXXU1BUE3
- Galaxy A32 — A325MUBU1AUD2
- Galaxy A50 — A505NKSU5DUD2
- Galaxy A51 — A515FXXU4EUD7
- Galaxy A72 — A725FXXU2AUE1
Simu za Galaxy S
Hapa orodha yake ni hii:-
- Galaxy S10e — G97xFXXUAFUE3
- Galaxy S10 — G97xFXXUAFUE3
- Galaxy S10+ — G97xFXXUAFUE3
- Galaxy S20 FE (4G only) — G780FXXS3CUD7
- Galaxy S20 FE 5G — G781BXXU3CUD6
- Galaxy S20 — G98xxXXU7DUDB
- Galaxy S20+ — G98xxXXU7DUDB
- Galaxy S20 Ultra — G98xxXXU7DUDB
- Galaxy S21 — G991BXXU3AUDA / G99xBXXU3AUE1 / G991USQU3AUDD (US)
- Galaxy S21+ — G996BXXU3AUDA / G99xBXXU3AUE1 / G996USQU3AUDD (US)
- Galaxy S21 Ultra — G998BXXU3AUDA / G99xBXXU3AUE1 / G998USQU3AUDD (US)
Simu za Galaxy Note
Simu ambazo zitapokea masasisho hayo ya mwezi Mei 2021 ni:-
- Galaxy Note 10 Lite — N770FXXU7EUE2
- Galaxy Note 20 — N986BXXU2DUDA / N981U1UES2DUD5 (US)
- Galaxy Note 20 Ultra — N980FXXU2DUDA / N986U1UES2DUD5 (US)
Simu za Galaxy Z na F (Foldable)
Hapa rununu zilizopo kwenye kundi hili (pamoja na zile zinazokunjika halikadhalika kukunjuka) ni:-
- Galaxy Z Flip 5G — F707BXXU3DUD7
- Galaxy Fold — F900FXXU5EUD7
- Galaxy Fold 5G — F907BXXU5EUD7
Masasisho ni muhimu sana kwenye rununu ama kifaa chochote cha kidijiti hivyo usipuuze.
Nilizoziorodhesha hapo juu ni simu za Samsung ambazo zitapokea/zimekwishapokea masasisho ya kiusalama kwa mwezi Mei 2021 na inawezekana kabisa rununu uliyonayo imeshapokea taarifa fupi na kama bado basi uwe mvumilivu kwani yatafika kwenye kifaa chako.
Vyanzo: Samsung, 9to5Google
No Comment! Be the first one.