fbpx
Apple, simu, Teknolojia

Simu mpya ya Apple iPhone 7 isiyo na ‘earphones’ za kawaida

simu-mpya-ya-apple-iphone-7-isiyo-na-earphone-jack

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Kampuni ya Apple imethibitisha kwamba simu yake mpya ya iPhone haitakuwa na tundu la kawaida la kifaa cha kusikiza sauti (Earphones), kwa Kiingereza hufahamika kama ‘audio jack’.

 Kuondoa tundu hilo la headphone ya 3.5mm kutanusuru nafasi inayoweza kutumiwa kuongeza vitu vingine
Kuondoa tundu hilo la headphone ya 3.5mm kutanusuru nafasi inayoweza kutumiwa kuongeza vitu vingine

Simu hiyo ya iPhone 7 badala yake itatumia teknolojia ya Apple ya lightning ambayo itamuwezesha mtu kutumia tundu moja kuunganisha simu na vifaa vingine.

Apple pia watavumisha kutumiwa kwa visilikizia sauti ambavyo havitumii nyaya, na imetoa aina yake ya earphone zinazojulikana kama Airpods.

Soma zaidi kuhusu iPhone 7

Sifa za Airpods

 • Airpods ni visikilizia sauti  vyenye ukubwa wa 3.5mm kilivumishwa sana na vicheza muziki vya Walkman vya kampuni ya Sony, lakini kilitumiwa mara ya kwanza katika redio zilizotengenezewa Japan mwaka 1964.
 • Zina uwezo wa kugundua zinapoingizwa masikioni. Hii inaziwezesha kusitisha uchezaji muziki zinapochomolewa masikioni.
 • Unaweza pia kuzielekeza kwa kutumia programu ya Siri. Hata hivyo, lazima ziwekwe chaji kivyake ingawa Apple inasema zinaweza kukaa na chaji kwa hadi saa tano. Kifaa chake cha kuhifadhia kinawezesha mtu kutumia kwa hadi saa 24.
INAYOHUSIANA  Kuna uwezekano wa utumiaji simu gizani kusababisha upofu! #Utafiti #Afya
Airpods-Earphones mpya kutoka Apple
Airpods-Earphones mpya kutoka Apple

Kampuni hiyo imesema imehitaji kutumia ujasiri kuchukua hatua hiyo. Hata hivyo, hatua hiyo huenda ikawaudhi baadhi ya wateja ambao sasa watahitajika kununua kifaa unganishi yaani adapter ndipo waweze kutumia visikilizia sauti.

Apple wamezindua iPhone 7 baada ya kipindi cha mwaka mmoja cha kushuka kwa mauzo ya simu za iPhone na kupungua kwa sehemu inayodhibitiwa na kampuni hiyo sokoni.

iPhone 7 pamoja na earphones ambazo ni wireless; Airpods.
iPhone 7 pamoja na earphones ambazo ni wireless; Airpods

Sifa nyingine za iPhone 7

 • Kitufe cha nyumbani sasa kinaweza kutofautisha uzito kinapobonyezwa na kutoa mtikisiko. Kitufo hicho sasa hakiingii ndani ya simu.
 • Simu hizo zinaweza kuingizwa ndani ya maji ya kina cha 1m (3.2ft) kwa dakika 30 wakati mmoja bila kuharibika
INAYOHUSIANA  Asus Zenfone 6: Simu ya kamera mbili kwa moja

Aina kubwa ya iPhone 7 Plus ina lensi mbili za kamera sehemu ya nyuma, ambayo inaimarisha uwezo wa kupiga picha.

dual-camera
Sehemu ya nyuma ya iPhone 7 yenye kamera 2

Bei ya iPhone 7

£599 hadi £799 ($799-$1,066)|Tsh 1,745,815-Tsh 2,329,210, kwa kutegemea uwezo wake wa kuhifadhi data. Kwa iPhone 7 Plus ni kuanzia £719 hadi £919 ($959-$1,226)|Tsh 2,095,415-Tsh 2,678,810.

Hiyo ndiyo iPhone 7 iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wengi. TeknoKona imekuhabarisha kama kawaida yake.

Vyanzo: BBC, the guardian

Facebook Comments

Sambaza
2 Comments
Share
Tags: , ,

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

2 Comments

 1. Mambo Makubwa Yaliyotangazwa Katika Tukio La Uzinduzi Wa iPhone 7!
  September 16, 2016 at 12:35 am

  […] […]

 2. iPod Touch 2019: Toleo la bei nafuu la iPod na kila kitu iPhone
  May 30, 2019 at 10:41 am

  […] pekee kinachokosekana katika iPod Touch ukilinganisha na simu kama iPhone 7 ni suala la uwezo wa kupiga picha, utambulizi wa sura (facial recognition) katika ufunguaji […]