fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Dell HP IBM Kompyuta Teknolojia Uchambuzi

Super Computer na Matumizi yake

Super Computer na Matumizi yake
Spread the love

Unazifahamu Super Computer? Teknokona leo tunakuchambulia maana, aina na matumizi mbalimbali ya aina hii ya kompyuta. Super Computer ni kompyuta zenye kiwango cha juu cha utendaji ukilinganisha na kompyuta za kawaida. Utendaji kazi wa kompyuta hizi unapimwa kwa uwezo wake wa kushughulikia kazi zilizosubirishwa kwa sekunde (FLOPS).

Kompyuta hizi huwa na maelfu ya prosesa ndani yake na zina uwezo wa kukokotoa mabilioni ya mahesabu ndani ya sekunde. Hutumika kuendesha programu zinazofanya kazi kwa muda halisi. Na nchi zinazoongoza kwa kuwa na kompyuta nyingi za aina hii ni Marekani, China na Ujerumani.

SOMA PIA  Intruder Alarm System; Fahamu kuhusu mfumo wa Ulinzi na Usalama

Super Computer hutumika kwenye madhumuni ya kisayansi na kihandisi yanayohitaji taarifa za kina na ukokotoaji mzito kama vile Quantum mechanics, utabiri wa hali ya hewa, uchunguzi wa mafuta na gesi, aerodynamics (Elimu ya Anga), utafiti wa nyuklia na uchanganuzi wa crypto (Sarafu za Kidigitali). Programu endeshi inayotumika sana kwenye kompyuta hizi ni Linux.

Super Computer

Picha: Muonekano wa Supa kompyuta za IBM 

Aina za Super Computer hutofautiana kutokana na matumizi yake pamoja na kampuni iliyotengeneza. Makampuni na mashirika yenye kompyuta hizi ni pamoja na IBM, HP, Fujitsu, SGI na Dell. IBM wametengeneza aina ya IBM Roadrunner, IBM Sequoia, IBM Blue Gene na IBM Power 775 .

SOMA PIA  Kadi janja kwa ajili ya Usafiri wa Mabasi ya Mwendo Kasi zaanza Kuuzwa

Endelea kutembelea tovuti yetu kufahamu zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake, Pia kupata habari mbalimbali za kiteknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania