Wiki hii iliyoisha imeshuhudia mambo mengi yakitokea hapa bongo, katika sekta ya habari kampuni ya Jamii media imeenda mahakamani kwenda kupinga baadhi ya vipengele vya sheria ya makosa ya kimtandao ambayo ilianza kutumika nchini kwaka jana mwezi wa tisa.
Ijue Jamii media.
Jamii media ni kampuni ambayo ndiyo wamiliki wa mitadandao mkiubwa ya Jamii forum na Fikra pevu, mitandao hii mikubwa miwili imekuwa ikichukua nafasi kubwa katika uchapishaji wa habari ambazo zimekuwa zinaibua ufisadi selikarini. Ufichuaji wa ufisadi wa Richmond ama Escrow kwa mfano ilichochewa kwa kiasi kikubwa katika mitandao hii, kwa namna moja au nyingine mitandao hii imekuwa ndilo jamvi la wafichua maovu selikarini ama kwa kimombo whistleblowers.
Jamii media wanapinga nini katika sheria ya makosa ya mitandao!?
Watu wengi wanadhani kwamba Jamii forum wanapinga sheria nzima ya makosa ya kimtandao hii sio kweli, Jamii media wamefungua shauri mahakamani kupinga vipengere viwili tu vya sheria hiyo ambayo ilipo sainiwa iliifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye sheria kali za makosa ya kimtandao.
Vipengere vya sheria ya makosa ya kimtandao vinavyopingwa na Jamii media ni vipi?
Jamii media inapinga vipengere vya 32 na 38 vya sheria ya makosa ya mtandaoni kwasababu vinapingana na ibara ya 16 na ibara ya 18 ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa maneno mepesi ni kwamba katika sheria hii ya makosa ya kimtandao kuna vipengere viwili ambavyo vinawapa polisi nguvu kutafuta taarifa za wahalifu wa kimtandao bila kupata kibali cha mahakama sasa hii inaweza kutumiwa vibaya na polisi kuwakamata wanaharakati wafichua maovu, hivyo kuvunja haki zao za kikatiba zinazowapa uhuru wa kujieleza na haki yao usiri.
Je ni kwanini Jamii media wameamua kwenda mahakamani kuvipinga vifungu hivi!?
Jamii Media wamefikia hatua ya kufanya haya baada ya kuwa wakipata maombi kutoka jeshi la polisi likiwataka kutoa taarifa za siri za wateja wake, wanadai kwamba kutoka kipindi cha uchaguzi Oktoba mwaka 2015 jeshi la polisi limekuwa likiwaandikia barua kuwashinikiza kutoa taarifa za siri za wateja wao.
Jamii Media wanadai kwamba wamekuwa wakipata mashinikizo kadha wa kadha wakitakiwa kutoa ama IP address ama taarifa nyingine za siri za wateja wao, na namna pekee wanaweza kuwalinda wateja wao ni kwa kuvipinga vipengere ambavyo vinawaruhusu polisi kuomba taarifa hizo bila ruhusa ya mahakama.
Ni matumaini yetu kwamba makala hii imekusaidia kuelewa kwa undani juu ya tatizo hili hasa vipengere hivi viwili vya sheria hii ya makosa ya kimtandao ambavyo vinalenga kutunyima haki yetu ya uhuru wa kujieleza na usiri. Tuwaunge mkono Jamii Media katika mapambano haya ya uhuru wa kujieleza ambayo ni haki yetu ya msingi.