Toyota kutambulisha gari lilotengenezwa kwa mbao na teknolojia ya kiutamaduni ya nchini Japan isiyohusisha utumiaji wa misumari wala nati katika kuzishikilia mbao hizo.
Teknolojia hii imetokea wapi?
Huko nchini Japan kuna mahekalu ya kitamaduni ambayo huvunjwa na kujengwa upya kila baada ya miaka 20. Kitu cha pekee katika ujengaji wa hekalu hizo no utumiaji wa mbao usiohusisha utumiaji wa ata msumari mmoja katika ujenzi wake.
Teknolojia hiyo inatumika kwa miaka mingi katika ujengaji wa hekalu maarufu Japan – The Ise Grand Shrine
Ubomoaji na ujengaji wa mahekalu hayo umekuwa ukifanyika kwa takribani miaka 1,300 sasa, na huwa wanabomoa na kujenga tena ili kuhakikisha majengo hayo yanaendelea kuwa na nguvu na usalama. Teknolojia ya ujengaji huo inapitia kwa vizazi hadi vizazi, na sasa Toyota wanatumia teknolojia hiyo katika utengenezaji wa gari.
Wiki ya Ubunifu mjini Milani, Italia
Takribani mwezi kuanzia sasa kutakuwa na maonesho ya ubunifu katika jiji la Milani, (Design Week in Milan, Italy) na ndio Toyota wanategemewa kutambulisha gari hilo rasmi.’
Ubunifu wa gari hilo ambao wameuita Setsuna, unaonesha kitu ambacho wanaweza kukifanya baadae. Wanashiriki maonesho hayo ili pia kuweza kupata mitazamo kutoka wabunifu wengine.
Aina kadhaa za mbao zimetumika kutengeneza bodi la gari hilo, chasis, viti, uskani (steering wheel) na rim za matairi.
Je mbao hizo zimejishakaje kama misumari na ‘screw’ hazijatumika?
Ni uunganishaji wa sehemu zinazokutana kwa kutumia maumbo ya ‘concave’ na ‘convex’ (umbo la mbonyeo) ndio vinavyoshikanisha sehemu mbalimbali za gari hilo.
Lini magari la namna hiyo litaanza kupatikana?
Usitegemee kununua gari hilo siku ya karibuni… ni kitu wanachokifikira kukifanya lakini si leo. Na ata hiyo miaka ya mbele wakitumia teknolojia hii kutengeneza magari ya kuingia sokoni na kuuzika yatakuwa ni magari ya bei ghari sana.