Tuendelee tuu kusubiri kuhusu Mate X kuingia sokoni

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kama kuna simu ambayo Huawei imepatanayo shida kwa mwaka 2019 basi ni Mate X ambayo ilizinduliwa zaidi ya miezi mitano iliyopita lakini mpaka hivi leo haijaanza kuuzwa.

Teknolojia ya simu zinazokunjika imerudi tena machoni pa watu na moja ya rununu ambazo zinauwezo huo ni Huawei Mate X lakini ipo wazi kabisa kuwa kampuni husika imekumbana na changamoto nyingi ambazo zimesababisha mpaka hivi leo simu hiyo haijapelekwa sokoni na taarifa zinasema bado haipo tayari kuweza kuanza kuuzwa.

INAYOHUSIANA  Logitech yanunua Kampuni ya vifaa vya Wireless, Jaybird

Mara kwa mara Huawei wamekuwa wapinzani wa karibu sana kwa Samsung ambao pia wana Galaxy Fold ambayo ina kitu kikubwa kisichopishana na mpinzani mwezake; kukunjika. Kutokana na kukawia huko kwa Mate X, Mkurugezi wa biashara ya mauzo yanayohusu simu janja kwenye kampuni husika, Bw. He Gang ni kwamba bado wanaendelea kuiweka sawa kabisa ili ifikie viwango vyao wanavyovitaka.

Mate X kuingia sokoni

Kwa mujibu wa tafsiri isiyo rasmi “Kila mtu afahamu kuwa kufikia kiwango ambacho kimewekwa  na Huawei ni kitu ambacho kinahitajika sana na iwapo haitaafikia basi bidhaa hiyo haitaweza kwenda sokoni”~Bw. He Gang.

Vilevile, inafahamika vyema kuwa Huawei wamewekeza nguvu nyingi sana kwenye bidhaa hiyo hivyo basi wanahitaji kuhakikisha bidhaa hiyo inakuwa sawa kwa asilimia zote kila idara kwa Huawei Mate X kuingia sokoni bila kufuata mkumbo wenzao wametoa simu basi na wao watoe.

INAYOHUSIANA  Zima "Automatic updates" kwenye simu yako

Kwa sasa tunachoweza kufanya ni kusubiri mpaka hapo itakapoonekana kuwa ni wakati sahihi kwa Huawei Mate X kuingia sokoni na kununulika.

Vyanzo: GSMArena, First Post

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.