Mkutano mkubwa wa teknolojia za mawasiliano duniani unaofanyikaga Barcelona (Mara nyingi) huwa unasababisha kutoka kwa bidhaa nyingi sana zenye ubora wa hali ya juu. Makampuni mbalimbali katika mkutano huo yanaonyeshaga maujuzi na maujanja mbalimbali kwa duniani nzima.
Lakini tangazo la SanDisk katika maonesho hayo limekua la aina yake, ni kitu kidogo lakini licha ya hivyo ni chenye ujazo (memory) mkubwa ndani yake. Wameleta kadi uhifadhi wa udogo wa ‘Micro SD’ yenye uwezo wa GB 200.
Katika utambulisho huo, SanDisk wameahidi kuwa SanDisk Ultra microSDXC UHS-I mpya toleo la ‘Premium’ itaweza kurekodi video zenye hali ya juu zaidi kwa masaa 20 na itaweza kuhamisha data kwa spidi ya 90 MB/s au picha 1,200 kwa dakika.
“Tunajikita katika teknolojia ili kuhakikisha wateja wetu wanapata viitu sahihi ambavyo vinawarahisishia matumizi ya simu zao’ -alisema Dinesh Bahal, Makamu wa raisi wa masoko wa SanDisk
SanDisk Ultra microSDXC UHS-I mpya toleo la ‘premium’ ni muendelezo wa SanDisk ya mwaka jana iliyokua na GB 128 ambayo pia ilivunja rekodi za memori kadi.
Wengi wanasema ingawa hili ni jambo kubwa sana kiteknolojia ila kuna wasiwasi ya kuwa kadi zenye ujazo mkubwa zinaathiri utendaji wa simu hasa za Android.
No Comment! Be the first one.