fbpx
Android, Android Pie, Samsung, Teknolojia

Samsung watoa masasisho ya Android Pie kwenye Galaxy J7 Duo

samsung-watoa-masasisho-ya-android-pie-kwenye-galaxy-j7-duo
Sambaza

Sio kila mwenye simu janja basi inatumia toleo la kenda kwenye mfumo endeshi kwa maana ya kwamba Android 9. Kuna mpaka hivi leo bado hazijapokea masasisho hayo hivyo basi kuendelea kusalia kwenye aina ya Android iliyopo kwenye simu husika.

Mara kwa mara Samsung wamekuwa wakitoa orodha ya simu ambazo zitapata sasisho la programu endeshi kwenye simu husika basi baada ya kuruhusu Android 9 kwenye Galaxy Xcover 4 mapema mwezi Julai 2019 Samsung Galaxy J7 Duo nayo pia imewezeshwa kuweza kuhamia kwenye toleo hillo la programu endeshi.

INAYOHUSIANA  Huawei kutoa mafunzo kwa wahitimu wa vyuo

Je, utahitaji nini?

Kimsingi unapotaka kushusha masasisho kwenye simu ni muhimu sana kuzingatia uimara wa intaneti (isiwe inakatikakatika), faili husika lina ukubwa gani na vilevile kwenye simu husika kuna kiasi gani cha intaneti. Sasa basi unatatakiwa kufahamu kuwa ili uweze kushusha Android Pie unatakiwa uwe na kifurushi cha intaneti kisichopungua GB 1.3.

Kwenye sasisho hilo kuna namna ambavyo programu zimepangwa kwenye Android 9 (UI 1.1) sambamba na kipengele cha muonekano wa giza.

Galaxy J7 Duo
Masasisho ya Android 9 kwenye Samsung Galaxy J7 Duo.

Kama simu yako ina uwezo mzuri tuu basi huna budi kuweka kifurushi cha intaneti ambacho kinatosha kisha ukaweza kushusha masasisho hayo kwenye simu janja husika vinginevyo utaendelea kubaki ukitumia toleo la nyuma wakati simu yako ya Android inastahili kupanda hadhi.

Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|