Ripoti zilizopo ni kwama simu ya iPhone 6s ndio inaleta wateja wengi katika kampuni kuliko toleo lake jipya yaani iPhone 7.
Toleo la iPhone 7 lilianza kupatikana rasmi septemba 2016. Ripoti zinasema katika msimu wa sikukuu (krismass na mwaka mpya) bei za vifaa vilishuka kama kawaida yake. Cha kushangaza ni kwamba watu walikimbilia iPhone 6s na kuacha iPhone 7.
Wengine wanakimbilia kununua iPhone 6s kwa sababu ina bei ndogo kuliko iPhone 7. Muandaaji wa ripoti hii Moskowitz amesema kwake yeye anadhani kuwa wateja wa simu janja washazoea kutumia simu janja hivyo mpaka wameshajiwekea katika vichwa vyao kuwa ‘Kuna toleo linguine bora zaidi ya hili”.
Hivyo basi wateja wanaona kuwa simu ambayo sasa hivi inapata jina sana na kuitwa nzuri baada ya muda inaweza ikawa ndio simu mbaya baada ya simu zingine kutoka.
TOFAUTI KATI YA iPhone 6s Na iPhone 7
Tofauti kubwa kati ya simu hizi mbili ni kama zifuatazo
• iPhone 7 ina prosesa iliyo na spidi zaidi
• Maberesho katika kamera
• Maisha marefu katika betri n.k
kwa kifupi ni kwamba maboresho haya hayajawa sababu (kwa kiasi kikubwa) kamili za kumfanya mteja abadilishe kifaa chake na kwenda kununua iPhone 7. Wengi wao sababu hizi zinawakimbiza mpaka kwenye iPhone 6s.
Kwa mwenendo wa sasa kutoa matoleo mengi mapya ya simu hakutaifanya kampuni ijipatie mapato mengi, lakini kama kampuni ikija na ubunifu maridadi basi haina budi kupata mafanikio makubwa.
Kitu kingine kikubwa kilichowafanya watu wabakie katika iPhone 6s ni kwamba ukiangalia kwa umakini utajua kwamba matoleo ya iPhone 7 hayajafanyiwa ubunifu mkubwa.
Vipengele vingi vya iPhone 6s vimerudishwa katika iPhone 7 hivyo hili limewafanya watu kujiuliza kwanza kabla ya kwenda kununa simu hiyo.
Ningepnda kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment hili umelipokea vipi? Je wewe unaona sababu hizi ni sahihi au unazo zingine kichwani?