fbpx

Mfumo wa QR Code unavyosaidia Watanzania

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Katika dunia ya leo wengi wetu tunatumia simu janja katika kufanya mambo mengi tu lakini mambo yalivyo hivi sasa mfumo wa QR Code unasaidia kurahisisha miamala duniani kote lakini hata kwa Tanzania.

Suala zima la muda na usalama wa miamala ni muhimu katika maisha ya kila siku hasa katika ulimwengu wa teknolojia na neno “QR Code” ni kawaida kwa yeyote yule anayependa kujua masuala ya teknolojia hasa inayotumika sana katika maisha ya kila siku. Mfumo wa QR Code unafanya kazi kwa kutumia kamera ya simu janja ambayo ina soma kilicho nyuma ya msimbo (CODE) na kisha kukamilisha malipo ndani ya muda mfupi.

INAYOHUSIANA  Tetesi: Muonekano wa simu mpya za iPhone

Taasisi nyingi nchini Tanzania zimeweza kuunganisha huduma zao kuruhusu miamala kufanyika kwa njia ya kutumia msimbo na kupunguza muda ambao angeweza kusubiri ili kuweza kufanya malipo; inaelzwa inachukua dakika mbili tu! kufanikisha muamala kwa njia hiyo ya kutumia simu janja kufanikisha malipo.

Mfumo wa QR Code

QR Code-njia rahisi inayotumia msimbo na simu janja kurahisisha malipo baina ya mteja na mfanyabiashara.

Ni ukweli usiopingika kuwa teknolojia ya msimbomilia imerahisisha uwezo wa kufanya miamala ndani ya muda mfupi na hasa ukizingatia watu wenye simu janja inazidi kuongezeka mwaka haaadi mwaka nchini Tanzania.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.