fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Jinsi Kompyuta Laptop Maujanja Teknolojia

Sababu Kwanini Hutakiwi Ku ‘Hibernate’ Laptop Yako!

Sababu Kwanini Hutakiwi Ku ‘Hibernate’ Laptop Yako!

Spread the love

Njia ya ku’Hibernate’ inaonekana katika ‘Operating system’ (OS) kama za Windows na hata OSX (MacBook). Hii njia yaku Hibernate inakusaidia kuisimamisha kompyuta (laptop) yako katika hali iliyoko ili baadae ukija kuwasha uendelee pale pale.

Mfano kama ulikua unaandika kitu katika Microsoft Word ukiwasha laptop yako basi utaendelee hapo hapo ulipoishia (Microsoft word). Hard disk ndio inahifadhi hali ulioiacha wakati una hibernate laptop yako. Nilikua natumia njia hii ya ku hibernate laptop mpaka nilipokuja kujua hasara zake… lakini kwa nini usi hibernate laptop yako?hibernate

Katika Windows utaona kabisa sehemu imeandikwa ‘hibernate’ lakini katika OSX (Macbook) utaona imeandikwa au imepewa jina la ‘safe sleep

SOMA PIA  7 za Kukufanya Mjanja zaidi Twitter

‘HIBERNATE’ INAFANYA NINI HASA?

Hibernate inaitwa ‘usingizi mzito’ kwa laptop yako. Kwa ufupi njia ya ku’hibernate itagandisha hali ya kazi inayofanya katika RAM ya laptop yako na kisha kuipeleka katika HARD DISK na kisha laptop kuzimika. Hibernate inawasha mashine (laptop) tofauti na njia ya kawaida ya kuwasha na inachukua muda kwa mashine hiyo kuwaka tofauti na ukiwa katika ‘sleep mode

hib

KWA NINI TUSITUMIE NJIA YA KU’HIBERNATE?

Baada ya kujua hibernate ni nini na nini kinafanyika mpaka inatokea laptop ina hibernate, hizi ni sababu ambazo zinakushauri usipende kutumia njia kwenye kifaa chako (laptop).

SOMA PIA  $150 hadi $0 : Programu ya Kuedit Picha ya Nik Collection sasa BURE, zawadi kutoka Google

Ku’hibernate laptop yako kutamaliza au kutatumia kiasi kikubwa cha betri pia kupunguza maisha ya betri la laptop yako. Pia ina athiri ‘system’ nzima ya ndani ya ndani ya mashine yako. Jiepushe na Njia hii lakini kama unatumia njia hii ya hibernate au sleep mode mara chache sana hiyo ni sawa maana njia hizi zimewekwa spesheli ili kutumika mara chache sana.

Sasa umejua kwa nini usiherbernate laptop yako?. Tumia njia yaku hibernate pale tuu inapobidi au jiepushe nayo ili kuongeza maisha ya laptop yako . Makosa kama ku’hibernate huku unaangalia muvi au huku kuna CD inayotumika katika laptop yanaweza kabisa kukuharibia mashine na hata hivyo itapata joto sana (kuchemka)

SOMA PIA  Waathiriwa wa Samsung Galaxy Note 7 wabadilishiwa simu

Inapokubidi kutumia ‘hibernate’ hakikisha unaweka laptop sehemu inayopata hewa vizuri. Hakikisha uifuniki au kuiweka kwenye begi au kuifunika kwa kitambaa au nguo ya aina yeyote.

Kuepuka kutumia njia hii kutafanya betri, eneo la CD na laptop yako kwa ujumla kudumu kwa muda mrefu zaidi.

Hivi ushatufikia katika kurasa zetu za Facebook, Twitter na Instagram? Unangoja nini!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

  1. Beatus KESSY - May 5, 2017 at 03:41 - Reply

    Page ya Telegram hamuiupdate kwa Taarifa siku hizi kwa nini?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania