fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android apps Intaneti simu

Tumia WhatsApp kwenye Kompyuta Yako Sasa

Tumia WhatsApp kwenye Kompyuta Yako Sasa

Spread the love

Kulikuwa na njia mbalimbali zisizo rasmi za kutumia WhatsApp kwenye kompyuta lakini sasa WhatsApp wamekuja na njia rasmi!

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji milioni 600 wa WhatsApp hii ni habari nzuri kwelikweli kama huwa unajikuta kazini unapata shida kila saa kutazama simu yako ili kujua umetumiwa nini. Hii ni habari njema kweli kweli kwa wafanyakazi na wengine wengi wanaokuwa wanatumia kompyuta kwa muda mwingi wa siku.whatsapp-234262

Je unaitumiaje?

SOMA PIA  Xiaomi yaendelea kukua kwa kasi

Kwanza hakikisha unatumia toleo jipya kabisa la WhatsApp, nenda kwenye soko la apps kwenye simu yako kuhakikisha hilo.

Hatua

1. Kwenye kompyuta yako, fungua Google Chrome kisha nenda https://web.whatsapp.com

2. Utaona kodi ya QR

Android/Windows/Nokia S60

3. Fungua app ya WhatsApp, Nenda Menu,  Chagua WhatsApp web.

SOMA PIA  FAHAMU: Huduma Ya 'Live Location' Ni Nini Katika WhatsApp Na Jinsi Ya Kuitumia!

Simu za BlackBerry

3. Fungua app ya WhatsApp, Nenda Chats,  Bofya Menu, Chagua WhatsApp web.

4. Kisha onesha simu yako kama vile unapotaka kupiga picha eneo la kodi ya QR kwenye https://web.whatsapp.com

Kutokana na vikwazo vilivyo kwenye simu za Apple (iPhones) bado wenye simu hizo hawataweza kutumia huduma hii kwa sasa. Pia kwa sasa hutaweza kutumia huduma hii kwenye Firefox, Internet Explorer na zingine zaidi ya Google Chrome tuu.

SOMA PIA  'Soma Baadae': Huduma ya Kukuokoa ukiwa Mtandaoni

Endelea kusoma Teknokona, usisahau kusambaza makala hii kwa ndugu na marafiki!

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. […] ya upatikanaji wa huduma ya WhatsApp kwenye kompyuta kupitia kivinjari cha kompyuta kama vile Chrome na Firefox sasa WhatsApp wameamua kuleta programu spesheli kwenye kompyuta – Windows na […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania