Moja kati ya vitu ambavyo makampuni mengi yanajihusisha na biashara ya kiteknolojia ni kuhakikisha kuwa bidhaa zake zinakuwa salama dhidi ya udukuzi, virusi na vitu vinginevyo vinavyoweza kuwa vibaya kwa bidhaa husika.
Google ambayo ni kampuni nguli na iliyoleta mengi mazuri imejipanga kufanya maboresho kwenye apps zake (Gmail na Google Drive) jambo litakalopelekea programu tumishi tajwa kuwa na ulinzi madhubuti.
Kwanini Google imeamua kuleta masasisho hayo sasa?
Kuna matukio mbalimbali ya kihalifu wa kitamtandao mbali na Urusi kuhusishwa na tuhuma za kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 huko Marekani. Jambo lingine ni uwezo wa wafuatiliaji wa kwenye mtandao wanaweza (third parties) kujua ni wavuti gani unapenda kutembelea.
Masasisho hayo ambayo yanatarajiwa kutoka Oktoba hii yatakuwa yenye uwezo imara ambao utazuia kabisa programu tumishi zenye uwezo wa kufuatilia kile unachofanya unapokuwa unaperuzi mtandaoni.
Tangu mwaka 2012 Google imekuwa ikitoa huduma ya kupata namba maaluma zinazowezesha mtumiaji kuingia kwenye akaunti yake ya Gmail baada ya kuingiza tarakimu hizo ambazo daima hazifanani (utakapoingia tena kwenye email yako tarakimu utazoingiza hazitofanana nazile ulizongiza mara ya kwanza).
Mpaka sasa masasisho hayo yamesifiwa na wengi na kuipongeza Google ambayo imekuwa ikifanya masasisho kwenye apps zake na kufanya watumiaji wa programu hizo kuwa salama kwa kiasi kikubwa. Wewe je, unauzungumziaje suala hili?
Vyanzo: MyBroadBand, The Verge
One Comment
Comments are closed.