Kwa lugha nyepesi Project Fi ni mtandao wa simu unaomilikiwa na Google ambao unafanya kazi kwa mtindo tofauti na mitandao mingine ambayo tumeizowea.
Mtandano huu unakupa huduma za simu za mkononi na huduma za intaneti kwa kutumia mitandao mingine, simu yako itachagua kutokana na mahali ulipo ni mtandao gani una shika vizuri na kisha kuutumia huo kupata huduma.
Kwa kutumia simu card maalumu ya Project Fi basi simu yako inaweza kupata huduma zote za simu ya mkononi (kupiga na kupokea simu, kutuma ujumbe ama huduma za intaneti) kwa kupitia mitandao mingine ambayo ina miundombinu kama minara na WiFi ambazo zimejiunga na umoja huo chini ya Google (Google wanaingia mkataba na makampuni hayo ya simu kuiwezesha huduma hiyo)
Unavyofanya Kazi
Mtandao huu unatumia simcard maalumu ambayo inaweza kushika mtandao zaidi ya mmoja( mfano Tigo Voda na Airtel) na pia inakuwa na programu maalumu ambayo inasaidia kuweza kuhama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine kutegemea na upatikanaji wa signal. Pia Project Fi inatumia mtandao kukupa huduma za simu ya kiganjani yaani hata ukiwa sehemu hakuna signal za mtandao wowote ukiunganisha na WiFi ukapata data basi utaweza kupiga simu na kutuma ujumbe.
Kuna tofauti gani na mitandao hii ya kawaida?!
Mitandao ya kawaida hutumia simcard ambazo zinauwezo wa kushika mtandao mmoja tuu na matokeo yake ni pamoja na simu kukosa mtandao pindi unapokuwa maeneo yasiyofikiwa na mtandao wako. Mitandao ya kawaida kama Smart Tanzania haitakupa huduma za kupiga na kupokea simu ama kutuma na kupokea sms kwa kutumia WiFi kitu ambacho mtandao wa Project Fi unakupatia.
Inapatikana nchi gani
Mpaka sasa Project Fi inapatikana katika nchi 120 na ukiwa katika nchi hizi unaweza kuwasiliana na kutuma sms bila ya kulipa malipo ya ziada kama ilivyozoeleka katika mitandao ya kawaida. Huduma hii hata hivyo bado ni kwa ajiri ya wale ambao akaunti zao za Google zimeandikishiwa kutoka Marekani, kwa sisi ambao tumeziandikishia hapa nchini itabidi zaidi.
Kwa sasa kuna kifurushi cha dola 20 za Marekani (takribani 42,000/=) mteja anapata dakika, na sms bila kikomo za nchini mwake (kwa sasa Marekani) na huduma ya sms nchi zote duniani bila kikomo.
Pia kwa sasa huduma hiyo inapatikana kwa watumiaji wa simu ya Motorola Nexus 6 na matoleo mapya lakini ni malengo ya Google huduma hiyo ipate kusambaa zaidi nje ya hapo.
Yote kwa yote huduma hii inasubiriwa na watu wengi ambao usafiri mara kwa mara, na pia katika mataifa kama yetu itakuwa faida kwani kuna baadhi mtandao wako unaweza ukawa na intaneti isiyo na kasi ukilinganisha na mitandao mingine.
Mbona hadi sasa sim hizo maalum hatujaziona?
Waliachana na mpango huu, wameweka nguvu zote katika simu za Google Pixels. Project Fi imebadilishwa na kuwa huduma ya intaneti ya faiba