fbpx

Kuhusu Google Pixel 3a na 3a XL sio fununu tena

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kwenye ushindani wa simu janja Google wameonekana kupata soko zuri tangu ilipoamua kuleta rununu za Google Pixel na tangu hapo wamekuwa wakitoa toleo bora zaidi kuliko lililopipita. Toleo la sasa (Pixel 3 na 3 XL) likiwa halina hata miezi sita sokoni, Google wameamua kukubali ni kweli Google Pixel 3a na 3a XL ndio simu zao zinazokuja.

Kwa wiki kadhaa imekuwepo minong’ono kuhusu Goole kutoa toleo jingine la simu za Pixel na kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa habari za zinazohusu simu janja sina shaka utakuwa umesomasoma mahali. Ndio, na katika hali ambayo haikutegemewa lakini ikiwa kama njia ya kukubali kile ambcho kimekuwa kikisemwa na watu Google kupitia tovuti yao rasmi wakaweka habari kuhusu simu zao na hapo ndipo walipozika minong’ono yote kuhusu Pixel 3a pamoja na vitu vingine ambavyo simu hiyo itakuja navyo.

Pixel 3a

Google walivyoamua kuweka wazi kuwa ni kweli Pixel 3a ipo.

Kufahamu ujio wa idhaa bila kujua sifa zake huwa haina mashiko sana na kulingana na vyazo vya kuaminika wameweza kuweka wazi sifa kuu za simu hizo mbil ambazo hazipo mbali kuzinduliwa.

INAYOHUSIANA  Vidokezo vya iPhone XR 2019

Sifa za Pixel 3a (sio rasmi)

Urefu+Ubora wa kioo: inchi 5.6 OLED (1080 x 2220)

Kipuri mama: Snapdragon 670

RAM+Memori ya ndani: GB 4/64GB

Kamera (nyuma): MP 12

Programu endeshi: Android 9 Pie

Nguvu ya betri: 3000mAh

Sifa za Pixel 3a XL (sio rasmi)

Urefu+Ubora wa kioo: inchi 6 OLED (1080 x 2160)

Kipuri mama: Snapdragon 670

RAM+Memori ya ndani: GB 4/64GB

Kamera (nyuma): MP 12

Programu endeshi: Android 9 Pie

Nguvu ya betri: 3000mAh

Simu hizo zinatazamiwa kuzinduliwa mwezi Mei 2019 ndio hapo tutaweza kujua kinagaubaga kuhusu sifa kamili za simu hizo. Kama wewe unavutiwa na simu za Pixel basi jiandae kununua toleo jingine.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.