Kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani rais wa Marekani ameachana na simu ya BlackBerry baada ya washauri wake kumruhusu kutumia simu janja ya aina nyingine.
Obama amekili kuanza kutumia simu mpya akizungumza katika kipindi cha Tonight show kinachoendeshwa na Jimmy Fallon na kurushwa na televisheni ya NBC.
Pengine kama raisi wa nchi yenye ushawishi mkubwa katika mambo mengi duniani nirahisi kufikiri kwamba Barack Obama anatumia simu ya kisasa zaidi lakini ukweli ni kwamba kwa muda mrefu Obama amekuwa anatumia Blackberry ambayo watu wengi wanaiona kama imepitwa na wakati.
>Kwanini Obama alichagua Blackberry!?
Hii ndio ilikuwa simu ambayo Obama alikuwa anaitumia kabla ya kuwa raisi na pamoja na pingamizi kutoka kwa baadhi ya watu aliamua kuitumia hata baada ya kuwa rais, simu hii ilifanyiwa baadhi ya mabadiliko kuiimarisha kiusalama.

>Je sasa anatumia simu gani?
Katika mahojiano na Jimmy Fallon rais huyo wa marekani anayekaribia kustaafu hakusema anatumia simu janja ipi kwa sasa (Pengine hajataka kusema kwa sababu za kiusalama), lakini ameiponda simu hiyo kwasababu anadai kwamba kwa sababu za kiusalaama watu wa usalama wameifungia na hawezi kupiga simu hawezi kutuma ujumbe, kupiga picha ama kusikiliza muziki.
Blackberry imekuwa ikianguka katika mauzo na ushawishi wake umezidi kushuka miongoni mwa watumiaji wa simu, makampuni mengi pamoja na mashirika ya umma ya serikali nyingi duniani ambayo yalikuwa yanatumia BlackBerry kama simu maalumu za ofisi yameacha na kuamia kwa za android na iPhone.