Je unazeeka na ngozi yako ya uso au mikono inaonesha uzee huo? Wanasayansi waja na ngozi ya bandia inayoweza wekwa juu ya ngozi ya kawaida na kuonekana kama halisi, na huku ikiwa haiathiriwi na kulowa n.k.
Kundi la wanasayansi kutoka chuo cha Harvard na M.O.T huko Marekani ndio walioweza kufanya jambo hili ambalo kwa wengi linaonekana kama vile limetoka kwenye filamu kuwa jambo la halisi, linalowezekana.
Hadi sasa watu 170 wamefanyiwa majaribio ya kujibandika ngozi bandia hii iliyopewa jina la ‘second skin’, yaani ngozi ya pili. Pia katika majaribio hayo imegundulika hakuna waliogundulika kupata madhara yeyote yale ya ngozi, hili likionesha ya kwamba malighafi (material) waliyotumia hayana madhara kwa ngozi za watu hao.
Wanasema kemikali zinazotumika kutengenezea ngozi bandia hiyo ni zile zinazokubaliwa ya kwamba ni salama zilizopitishwa na Bodi ya Chakula na Madawa ya Marekani.
Ngozi hii bandia ni ‘transparent’, na hivyo ni vigumu kugundulika kama mtu ameweka kitu chochote juu ya ngozi yake. Inaweza valiwa siku nzima bila kusababisha muwasho wowote na inaweza kuhimili jasho na mvua. Utaweza nawa n.k bila kuathiri chochote, haitotoka.
Inasemekana matajiri wengi ambao uzeeka uchagua kufanya oparesheni za kuweka nyuso zao vizuri. Kuvuta na kupunguza ngozi ili kuzipa nyuso muonekano wa ujana. Njia hii isiyohusisha oparesheni inaonekana inaweza ikawa ndio njia bora na rahisi zaidi kufanyika.
Inasemekana matibabu ya magonjwa kama vile Eczema na Psoriasis yatanufaika na teknolojia hii
Matumizi mengine yanayoonekana yatawezekana ni pamoja na kutumia ngozi hii bandia kushikilia dawa iliyopakwa katika sehemu ya ngozi. Yaani dawa itapakwa kwenye eneo la ngozi na kisha ngozi bandia kuwekwa juu yake.
Inawekwaje?
- Itakuwa kwenye mfumo wa ‘cream’, yaani kama mafuta ya ngozi. Kuna mchanganyiko wa mafuto hayo, utapaka ya kwanza kisha kupaka nyingine juu yake…baada ya kukaa kwenye ngozi tuu itabadilika na kuwa ngozi ya bandia.
Angalia video hii fupi inayoonesha teknolojia hiyo…
Je una maoni gani juu ya teknolojia hii?
Soma Pia – Uwezekano wa kurudisha uhai kwa marehemu! #Teknolojia
Vyanzo: BBC na The New York Times