fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Tanzania

Nenda Paris Ukiwa na Boom J8: Tecno Tanzania waja na shindano!

Nenda Paris Ukiwa na Boom J8: Tecno Tanzania waja na shindano!

Spread the love

Kampuni ya simu ya TECNO Mobile wamekuja na shindano linalohusisha simu yao mpya iliyoingia sokoni ya Tecno Boom J8. Katika shindano hilo lililopewa jina la #BoomJ8ParisTZ mshindi atapata nafasi ya kusafiri hadi jiji la Paris nchini Ufaransa.

tecno boom j8 paris

‘Paris ni moja kati ya miji mashuhuri ulimwenguni kote ukiwa na vivutio mbali mbali. Ukiwa umeshikilia namba mbili ya miji inayovutia zaidi ulimwenguni umekuwa ukitembelewa na watu kutoka mataifa mbali mbali kila mwaka.

SOMA PIA  Tanzania yajenga Kituo cha Data (Data Center) kikubwa zaidi Afrika Mashariki

Kwa kupitia Boom J8 unaweza kushiriki katika shindano la #BoomJ8ParisTz kwa kushare wimbo unaupenda zaidi kutoka katika Boom Player kwenda katika ukurasa wako wa Facebook. Ukishafanya hivyo kilichobaki ni kuwataarifu washikaji waweze kulike.

Kushiriki ni rahisi na kushinda pia hakuhitaji kazi ngumu, kila siku mtu mmoja anajishindia Boom J8 mpyakwa kushare wimbo aupendao kutoka Boom Player, lakini pia kuna zawadi nyingine kibao.

SOMA PIA  M-Paper: App ya Tanzania Inayokupatia Magazeti Mbalimbali Kwenye Simu/Tableti Yako

Boom J8 imekuja na maajabu ambayo hutaacha kuipenda kila siku, kama unataka kwenda Paris itakapofika tarehe 23 Mei, Basi bonyeza http://goo.gl/qh78WU kushiriki katika shindano.’ – ilisomeka taarifa rasmi

Tupo njiani kuweka uchambuzi wa simu hii ya Tecno Boom J8 ndani ya wiki hii. Ingawa Tecno wanafamilia zingine za simu kama vile Phantom na Camon, simu za Boom zinawakilisha familia ya simu zinazowalenga wapenda muziki zaidi.

SOMA PIA  Mfumo wa kugundua TB kwa njia ya simu

Je ushainunua au kuiona tayari? Tuambie ni kipi kimekuvutia katika simu hiyo?

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. […] [Soma Pia -> Kuhusu shindano linalohusisha Boom Player ambalo mshindi atapelekwa nchini Ufaransa katika jiji la …} […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania