Sayari ya Zebaki leo imefanya jambo adimu ambalo hutokea walau mara 13 katika karne, sayari hiyo ambayo wengi tunaijua kwa jina la kimombo yaani Mercury leo imeonekana na wakazi wa miji mingi duniani ikipita mbele ya jua kitendo ambacho hakitajirudia tena mpaka Novemba 11 mwaka 2019.
Kutokana na jinsi mzunguko wa dunia kulizunguka jua ulivyo na pia jinsi mzunguko wa Zebaki kulizunguka jua basi kuna siku kumi na tatu ama kumi na nne pekee (katika miaka 100)ambapo Dunia Zebaki na Jua vinaweza kuwa walau katika mstari mmoja, siku hizi zinaweza kuangukia mwezi Mei ama mwezi wa Novemba.
Mara ya mwisho tukio kama hili lilitokea mwaka 2006 na pengine kama unawaza ni kwanini wanasayansi duniani kote wanafuatilia jambo hili, kupitia kuiangalia Zebaki ikikatisha katika uso wa dunia yapo mambo mengi ambayo wanasayansi ambao wanaliangalia tukio hili wanajifunza juu ya tabia za sayari hiyo iliyo karibu zaidi na jua (Mambo amabayo wanasayansi wanajifunza kwa kuangalia sayari hii inapopita katikati ya jua na Dunia ni maada ndefu ambayo pengine Teknokona itaijadili siku zijazo).
Kwa sababu za muundo wa Dunia Zebaki na pia Jua tukio hili halitaonekana kila mahali duniani bali baadhi ya maeneo tuu (Tanzania sio moja ya nchi ambazo zitaweka kuliona tukio hili lote ila kiasi fulani cha tukio hili kilionekana mida ya saa nane hadi saa kumi na mbili), lakini kwa faida ya ambao hawajui ili kuangalia tukio hili basi ilibidi mtu uwe na kifaa maalumu cha kulinda macho maana ukiangalia kwa macho ya kawaida basi ingekusababishia madhara kwa macho yako.
Mambo manne mengine ambayo ni muhimu kuyajua juu ya sayari hii ya Zebaki.
- Sayari hii ndio ndogo zaidi kuliko zote na pia ndiyo sayari iliyo karibu zaidi na jua.
- Sayari hii inatumia siku karibu 90 kulizunguka jua, na kama ilivyo kwa dunia sayari hii inazunguka katika muhimili wake kwa kutumia muda wa siku zipatazo 59.
- Sayari hii itaonekana ikikatisha mbele ya Jua kwa muda upatao wa masaa saba na nusu (Lakini sio kwa kila eneo wataona tukio zima kwa mfano Tanzani tukio hili lilidumu kwa masaa takribani manne)
- Sayari hii itakatisha tena mbele ya jua (ikiangaliwa kutoka katika Dunia ) 2019, 2032, na 2039.
Makala hii imeandikwa kwa msaada vyanzo mbalimbali mtandaoni kama vile mtandao wa Time and Date