fbpx
Teknolojia

Kampuni tanzu tatu za Sony kuwa kitu kimoja

kampuni-tanzu-tatu-za-sony-kuwa-kitu-kimoja

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Duniani kote wanafahamu moja ya kampuni nguli inajishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za kieletroniki ambazo zimekuwa zikiuza wanachotengeza nchi nyingi tuu ulimwenguni, hapa nazungumzia Sony Electronics Corporation.

Sony wamekuwa wakitengeneza vitu vingi ambavyo vimekuwa vikipata soko na kuingizia faida kampuni hiyo ambayo imekuwa ikileta ushindani kwa wapinzani ambao nao wanajihusisha na shughuli hiyohiyo lakini kuanzia Aprili Mosi 2020 kampuni tanzu takribani tatu (3) ambzo zinabeba jina la Sony; namaanisha Sony Mobile Communication, Imaging Products & Solutions and Home Entertainment & Sound. Kwa tafiri isiyo rasmi kampuni hizo tanzu ni ile inajishughulisha na utengenezaji wa simu, kamera na vifaa vya kieletroniki mahususi kwa majumbani ambapo kuanzia tarehe iliyotajwa zitakuwa chini ya mwamvuli mmoja.

Sababu ya uwamuzi huo inaaminika kuwa kampuni hizo zimekuwa zikishindwa kujiendesha vizuri kutokana na kutopata mapato mengi yanayokidhi wao kuweza kujitegemea.

Kampuni tanzu
Kampuni tanzu za Sony: Moja ya bidhaa ambazo zitakuwa chini ya kapu mmoja.

Hata hivyo, Sony Interactive Entertainment amabyo inategeneza Playstations na magemu mbalimbali kutumika kwenye kifaa hicho yenyewe haitaunganishwa na wenzake kwa maana kwamba wao wataendelea kujiendesha kivyao ambao kimsingi wameonekana kuendelea kufanya vizuri kibiashara.

Kampuni tanzu
Kifaa cha kucheza magemu kutoka Sony.

Maamuzi ya kuzileta kampuni tatu za Sony sehemu moja yanalenga kuziongezea mauzo/uwezo wa kujitangaza, kupata wateja, n.k na hatimae kuifanya kiongozi mkuu anayezibeba zote kujiongezeaa mapato. Je, wewe ni shabiki wa bidhaa za Sony?

Vyanzo: GSMArena, SRN

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Windows 10 Kuuzwa katika USB - Flash Disks
0 Comments
Share
Tags: , , ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|