Siku chache zilizopita tuliandika kuhusu Microsoft kuamua kutengeneza tablet wenyewe itakayotumia Windows 8, ‘Surface’, na habari moto kwenye intaneti ni kuhusu kampuni ya Google nayo kuleta tablet wanayoisimamia utengezaji wake wote kwa ushirikiano na kampuni ya Asus.
Tablet hiyo itaitwa Nexus 7, 7 imetokana na kuwa na ukubwa wa inchi 7. Tofauti na Microsoft ambao watatengeza ‘tablet’ ya Surface wenyewe Google ameshirikiana na kampuni ya Asus, ila logo ya kifaa itaitwa Nexus (hili ndo jina la kibiashara katika bidhaa kama simu ambazo hutengenezwa na Google).
Usichanganye tunavyosema hii ni atua ya kitofauti, katika tablets na simu zingine zitumiazo Android kama ilivyo kwa kompyuta zitumiazo Windows ni kwamba Google na Microsoft wamekuwa wanatengeza ‘operating system’ na kisha makampuni mbalimbali kama Samsung, HTC, Asus, na zingine huchukua na kutengeneza vifaa hivyo. Kwa upande wa utumiaji wa Windows makampuni haya huilipa Microsoft takribani dola 60 kwa kila kifaa kitakachotumia Windows, wakati Android itolewayo na Google huitoa bure kwa makampuni haya.
Ndo maana ingawa kuna tablets mbalimbali zitumiazo Android (OS ya Google) ila kampuni ya Google haikuwahi kusimamia na kutoa tablet na hii ndo itakuwa ya kwanza kama ilivyo kwa Microsoft wanaotegemea kutoa tablet ya Surface hapo mwakani.
Add caption |
Nexus 7 itakuwa na matoleo mawili, moja la gb 8 na jingine gb 16, pia itakuwa na RAM ya gb 1. Itakuwa na betri ya uwezo wa kukaa masaa 8 katika utumiaji baada ya kuichaji. Na itatumia toleo la hivi karibuni la Android nalo ni Android 4.1 kwa jina jingine ‘Jelly Bean’, hili limekuja baada ya toleo la ‘Ice Cream Sandwich’. Ni itakuwa nzuri zaidi kwa matumizi kama ya kusoma vitabu vya elektroniki (ebooks), kutumia intaneti, kucheza gemu na kuangalizia video. Kwa lugha ya kiingereza tunaweza sema ni kifaa kizuri kwa ajili ya ku’consume’ na sio kwa ajili ya ‘creation of materials’.
Nexus 7 |
Tablet ya Kindle Fire |
Watafiti wengi wanaamini Nexus 7 itashindana na tablet nyingine itumiayo Android inayofanya vizuri zaidi katika soko, Kindle Fire. Nguvu ya juu kwa Nexus 7 dhidi ya Kindle Fire ni pamoja na kuwa na toleo jipya zaidi la Android kulinganisha na Kindle Fire.
Tablet hii inategemewa sokoni ndaniSiku chache zilizopita tuliandika kuhusu Microsoft kuamua kutengeneza tablet wenyewe itakayotumia Windows 8, ‘Surface’, na habari moto kwenye intaneti ni kuhusu kampuni ya Google nayo kuleta tablet wanayoisimamia utengezaji wake wote kwa ushirikiano na kampuni ya Asus.
Tablet hiyo itaitwa Nexus 7, 7 imetokana na kuwa na ukubwa wa inchi 7. Tofauti na Microsoft ambao watatengeza ‘tablet’ ya Surface wenyewe Google ameshirikiana na kampuni ya Asus, ila logo ya kifaa itaitwa Nexus (hili ndo jina la kibiashara katika bidhaa kama simu ambazo hutengenezwa na Google). ya wiki mbili, na ya gb 8 inatemewa kuuzwa kwa dola za kimarekani 199, au takribani Tsh 310,000/= na ya gb 16 itauzwa dola za kimarekani 249, takribani Tsh 390,000/=.
“Kuna tetesi kuwa hapo kampuni ya Google imeanza mchakato wa kutengeneza toleo la inchi kumi la Nexus, litakoloitwa Nexus 10, hadi sasa hizi taarifa hazijathibitishwa na wao”
Teknokona tunakutakia Wikiendi njema!!!
No Comment! Be the first one.