Tulishaandika kuhusu uamuzi wa ajabu uliochukuliwa na mtandao wa kijamii wa Facebook wa kubadilisha anuani za barua pepe katika profaili za watu wote.
Hatua hii inafanya watu mbalimbali waliokuwa wanategemea kuunganisha program zao kama simu, laptop na huduma zingine katika kupata data muhimu kama barua pepe za watu wamekuta vitabu vya anuani (address book) zimebadilishwa.
Kwa mfano kama simu yako ilikuwa inajaza taarifa zingine muhimu kama anuani za barua pepe za watu kutoka Facebook, mfano kama simu za Blackberry, IPhone na nyingi za Android, basi uwe makini kwa sasa kabla ya kumtumia mtu barua pepe.
Kwani anaweza asizipate kabisa, na zikienda zitatumwa @facebook.com , na kama ni ya kikazi ujue mambo hayatakuwa official tena. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kutatua hali hii soma makala yetu kwa kubofya hapa http://teknokona.com/2012/06/facebook-wabadilisha-anuani-ya-barua.html na usisahau ku’share’ makala hii na wengine!
No Comment! Be the first one.