Vifurushi vya BIS ndiyo watu wangu huwa wanazungumzia kama BBM, lakini huwa wanakosea. Ulipii huduma ya BBM (Blackberry Messenger) bali unacholipia huwa ni huduma ya BIS (Blackberry Internet Service), ambayo ukishajiunga unapata mlolongo wa huduma nyingine nyingi za intaneti katika simu yako ya Blackberry kama kuweza kutumia huduma ya kuchati ya Blackberry (BBM), huduma za barua pepe, kutumia programu maarufu za simu kama Facebook, Twitter, Opera, Whatsapp na zingine nyingi.
Watu wengi huwa wanajikuta wakinunua simu za Blackberry bila kuelewa mfumo wake wa malipo. Watengenezaji wa Blackberry, kampuni ya RIM (Research In Motion) wamezijengea simu hizi ulizi mzuri wa huduma za intaneti (encryption) ili watumiaji waweze kujua data zao zipo salama na pia ata kama pale utakapofuata data zako muhimu uweze kuzipata. Kwa kifupi ni mfumo uliofumwa vizuri sana kiasi ya kwamba simu hizi mawasiliano yake ya intaneti lazima yapitie katika kompyuta kuu za RIM, na kupitia huduma hizi ndio maana makampuni ya mawasiliano yanabidi yaweke malipo ya vifurushi. Katika pesa hizi tunazolipa kuna asilimia inabaki kwa kampuni husika ya mawasiliano na nyingine inaenda kwa RIM.
Baada ya kuelewa kwa ufupi kwa nini watumiaji wa Blackberry inawabidi kulipia huduma za intaneti kwa mfumo huo tuje katika sehemu hii; ITAKUWAJE PALE AMBAPO WEWE HUTAKI KUTUMIA HUDUMA NYETI ZA BIS KAMA MFUMO WA BARUA PEPE NA BBM?
Kila mtandao wa simu unaweza ukawa umekaba kivyake kufanya wenye Blackberry waingie mikataba ya vifurushi. Lakini kivinjari (Browser) cha Blackberry kinatakiwa kufanya kazi ata kama ujajiunga katika vifurushi vya BIS, itategemea wewe unatumia mtandao gani, kuna baadhi ya mitandao unakuta usipojiunga huduma ya BIS huwezi kutumia programu maaraufu za simu kama Whatsapp, UberSocial, na Opera/OperaMini.
Hapa chini nitakufundisha jinsi ya kuzifanya huduma hizi zifanye kazi {kwangu nimefanya hivi na napata huduma za intaneti kwenye kivinjari cha Opera, Whatsapp na programu maarufu ya Twitter ya UberSocial. Siwezi kukupa asilimia mia kuwa zitakubali kwako ila zijaribu na uhakika kwa wengi matokeo yatakuwa chanya!}.
Na kumbuka simu yangu inatumia toleo la Blackberry la 6, modeli 9700.
1.Nenda kwenye menyu/orodha kuu.
Baada ya hapo nenda na ingia ‘Options’
2.Ukifika hapo nenda na ingia ‘Device’
3.Alafu nenda na ingia ‘Advanced System Settings’
4.Baada ya Hapo nenda na Ingia ‘TCP IP’
5.Baada ya hapo, utakuta menyu kama hii hapa chini,
Chagua kiboksi cha kuwezesha APN kama nilivyofanya hapa chini,
alafu kwenye APN andika ‘internet’, kumbuka usiweke hizo alama za ‘ na ‘.
Baada ya hapo zima, toa betri la simu na kurudisha. Simu ikiwaka jaribu kutumia
huduma mbalimbali ambazo ulikuwa uwezi zipata bila kulipia kifurushi cha BIS.
Ukifanikiwa tutafurahi kusikia kutoka kwako,
na kama unajua njia nyingine ya kufanikisha hili tueleze pia.
No Comment! Be the first one.