fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta Microsoft teknokona Teknolojia Windows

Vitu Kwenye Windows Ambavyo Microsoft Hawawezi Kuvijibu!

Vitu Kwenye Windows Ambavyo Microsoft Hawawezi Kuvijibu!

Spread the love

Microsoft_2014_windows10Je unafahamu ya kuwa kuna mambo mengine ambayo hayataenda kawaida kama ukiyajaribu kwenye kompyuta yako ya Windows? Yasome hapa kuyafahamu vizuri;

#1. Najua kila mtu anaweza tengeneza folder mpya kwenye kompyuta yake. lakini hilo sio tatizo tatizo ni kwa kuna majina kadhaa ukiya weka katika folder jipya, litagoma halitakubali kujitengeneza. Baadhi ya majina hayo ni CON, PRN, AUX, CLOCK$, NUL, COM1, COM2, COM3, COM4, COM5, COM6, COM7, COM8, COM9, LPT1, LPT2, LPT3, LPT4, LPT5, LPT6, LPT7, LPT8, and LPT9Mara ya kwanza nilizani au kwa sababu maneno mengi hayo yana herufi nne au tatu tuu? lakini hapana unaweza tengeneza ma folder mengi kwa herufi tatu au nne.  Jaribu sasa na hutaweza tengeneza folder likiwa na majina hayo. Hii ni ya ajabu sio?

SOMA PIA  Njia rahisi ya kupata PUK ya kadi yako ya simu

Untitled

#2. Pia hiki ni kitu kinachofurahisha ambacho ni vigumu kuki elezea?. Timu nzima ya microsoft hata Bill Gates mwenyewe walishindwa kuelezea nini kimetokea. iligunduliwa na programa wa kibrazili, jaribu mwenyewe uone. fungua microsoft word na kisha andika =rand (200, 99) na kisha bonyeza enter, subiri! unaona uchawi?. Hiyo ni virus au? yametokea maneno kwenye page zaidi ya 400.

Untitleddf

 

#3. Nina imani mnaijua namba ya ndege moja kati ya zile ndege ambazo ziligonga moja kati ya WTC towers  U.S na Osama Bin Laden katika 9/11 ambayo ilikua ni Q33N. Katika Notepad / WordPad au  Microsoft Word andika hiyo namba ya ndege Q33N kisha ongeza ukubwa wa maneno hadi 72 alafu badilisha muandiko uwe Wingdings. Utashangazwa kuona hii. Utaona picha ya ndege, majengo mawili na ,mbele yake kukiwa na alama ya Hatari (danger). Hii imetokea kabla hata ya 9/11, microsoft inabidi waweze kujielezea kwa hili

SOMA PIA  Linkedin waanzisha mtandao wao wa vipindi vilivyo katika mfumo wa sauti

Untitled

 

Ushawahi fikiria kwamba kompyuta itashindwa fanya kitu kidogo kama kulipa folder jina la “CON”?. Teknokona anaendelea kukujuza zaidi. Tembelea kurasa zetu za Twitter, Facebook naInstagram  tafadhali

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania