Hivi ushawahi kujiuliza kama unaweza kupiga simu kutoka kwenye kompyuta kwenda kwenye simu? kama unajiuliza hilo, ndio! unaweza lakini tatizo ni dogo kwa sababu lazima uwe umejiunga na internet tofauta na huduma za kawaida za kupiga simu kama kwa kutumia tigo,vodacom na airtel na pia kifaa chako (simu) lazima kiwe na uwezo wa kupakia viber.Labda wewe sio mpenzi wa whatsapp basi hii pia ni kwa ajili yako.
Viber ni App ya bure na inapatikana katika masoko yote ya simu yaani Android,iOs, App world na windows phone. Os zinazosapoti ni iOs 4.3 au za mbele ,Android 2.0 au za mbele, Windows Phone 7.5 au mbele na Blackberry 5.0.0 au za juu zaidi.
SOMA PIA: Shusha, Wezesha, Tumia WhatsApp Kwenye Kompyuta Yako!
Install Viber Katika Simu Yako.
Hii haina haja sana ya kuelezea ni inabidi tuu kuingia katika soko la kushusha app na ushushe viber
- Kwa Android —————->> Bofya hapa
- Kwa Windows Phone —->> Bofya Hapa
- Kwa black Berry ————>>Bofya Hapa
- Kwa NOKIA——————>>Bofya Hapa
Shusha Viber Kwa Kompyuta: NJIA YA KWANZA
Kuna Njia ya kushusha viber moja kwa moja kwenye kompyuta yako kwa aina zote mbili yaani Windows na Mac Os
- Watumiaji wa Windows: Bofya Hapa ili kushusha Viber.
- Watumiaji wa Mac Os: Bofya Hapa ili kushusha viber.
- Mara baada ya kukubali click viber na anza instillation katika komyuta yako
- sasa umeweza kuinstall viber katika kompyuta yako
- baada ya kumaliza intillation Sasa click katika alama ya viber ili kuifungua
- fuata maelekezo machache kwa kujaza taarifa zako muhimu, kisha itakua tayari kwa matumizi
Shusha Viber Kwa Kompyuta: NJIA YA PILI
Tumia viber kwa kompyuta kwa kutumia bluestacks. kama unataka kuwa na app mbali mbali za Android katika kompyuta yako basi hauna budu kushusha ’emulator’ mbali mbali za Android. Moja kati ya emulator zinazojulikana sana ni Bluestacks.
- download na install bluestacks katika kompyuta yako
- ukishamaliza instillation nenda katika sehemu ya kutafuta app
- tafuta App ya Viber Katika sehemu hiyo ya kutafuta App
- ikitokea ibofye alafu ishushe
SOMA PIA: Sasa Unaweza Kumuona Unayempigia Simu na Viber
Viber ni moja kati ya App nzuri zinazomuwezesha mtumiaji kupiga, kupokea na kutuma ujumbe mbali mbali katika simu na kompyuta yako. Hii ni Kama whatsApp lakini ikiwa na vitu vingi vya ziada kuliko whatsApp,
Tembelea kurasa zetu za Twitter, FacebooknaInstagram tafadhali.
No Comment! Be the first one.