fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Microsoft Teknolojia

Microsoft yafanya Majaribio ya Kituo cha Data chini ya bahari

Microsoft yafanya Majaribio ya Kituo cha Data chini ya bahari

Spread the love

Microsoft wamefanya jaribio la kuweka kituo cha Data (kilichopewa jina la Leona Philpot)  chini ya bahari. Katika jaribio hilo kituo cha data cha mfano kilitumika ambapo server ziliwekwa ndani ya chombo kisicho pitisha maji ambacho kilizamishwa chini ya bahari.

Leona Philpot

Leona Philpot ikiwa tayari kuzamishwa baharini

Misheni ya majaribio haya imepewa jina la Project Natick  na chombo chenyewe kimepewa jina la Leona Philpot kina kipenyo cha futi nane ambapo chombo hicho kimewekwa chini ya bahari ya Pacific umbali wa futi 30 kutoka juu.

SOMA PIA  Tegemea Mambo Haya Katika Toleo La iOS 11! #MaelezoNaPicha

Chombo hicho kimekaa ndani ya maji kwa siku 105 kwa majaribio kikiwa kinaongozwa kutoka katika ofisi za Microsoft, na ili kuelewa mazingira chini ya bahari chombo hiki kimefungwa sensor ili kupima mambo mbalimbali kama joto mgandamizo na unyevunyevu.

Kwanini jina hili?

Pengine unawaza kwanini microsoft walikipa chombo hicho jina hili, Leona Philpot ni jina la mmoja wa washirika wa gemu ya halolens, project nyingine ya Microsoft.

Kwanini baharini?

Ili kukiendesha kituo cha Data bila shida yapo mambo mengi ambayo ni lazima yawekwe sawa na pamoja na yote ni kuhakikisha kwamba kituo cha data kipo madhingira yanayo ruhusu mitambo hasa kompyuta inapoozwa vizuri. Vituo vya data huumia nguvu nyingi kupoooza mitambo na ndio maana vituo huwekwa katika mazingira yenye baridi ili kuwezesha upoozwaji wa kiwango kikubwa.

  • Baharini kuna hali ya ubaridi ambaayo haibadiriki saana kutegemea na vipindi vya mwaka hivyo itasaidia zaidi upoozaji.
  • Baharini pia kunauwezekano wa kuzalisha nishati mbadala ambayo inatokana na Upepo na pia Mawimbi ya bahari hii itasaidia saana kupunguza gharama za kuendesha vituo hivi vya data.
SOMA PIA  Kampuni tanzu tatu za Sony kuwa kitu kimoja

Soma Pia: Statoil kujenga mradi mkubwa zaidi wa kufua umeme baharini

  • karibu watu bilioni 3.5 wanakaa ndani ya maili 125 kutoka baharini hii inafanya kuwa na kituo cha data baharini kutawezesha watu wengi zaidi kufikiwa na huduma za internet

Hata hivyo bado zipo changamoto nyingi ambazo microsoft watakutana nazo pindi watakapo taka kuanza kutengeneza vituo vya data chini ya bahari, moja ya changamoto hizi ni madhingira. Ni ukweli usiopingika kwamba kuweka kituo cha data chini ya bahari itasababisha madhara kwa sio tu madhingira bali hata viumbe ambavyo vinazungukia madhingira hayo.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania