fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Microsoft Tablet Windows 8

Microsoft Waleta Tableti Mpya ya Surface Pro 3!

Spread the love

Surface Pro 3

Kampuni ya Microsoft hii leo wametambulisha tableti mpya (Surface Pro 3) yenye ukubwa zaidi wa upana na urefu kuliko matoleo ya nyuma. Surface Pro 3 inaupana wa inchi 12 kutoka 10.6, tableti hii wanaipa sifa ya kuwa na uwezo mkupya wa kushindana vikali na laptop katika uwezo wa ufanyaji kazi. Ikiwa na wembamba wa milimita 9.1 imekuwa ndiyo kompyuta/tableti nyembembe zaidi inayotumia ‘proccesor’ za Intel kuwahi kutengenezwa duniani.

Tokea Microsoft walete tableti ya kwanza ya Surface mwishoni wa mwaka 2012 bado hawajapata mafanikio makubwa kulinganisha na makampuni kama Apple kupitia iPads au Samsung kupitia Galaxy Tab. Kupitia toleo hili wanaendelea kufanya maboresho kwa kuzidi kuzipa uwezo mkubwa zaidi tableti zao. Surface Pro inakuja na Windows 8 na mtumiaji atakuwa na uwezo wa kutumia programu mbalimbali ambazo amezoea kutumia katika laptop au kompyuta ya kawaida ya Windows.

SOMA PIA  Android 5 Lollipop Yaja na Swichi ya Kuua Simu

Katika kuwahakikishia wafanyabiashara na wafanyakazi kuwa Surface Pro ndiyo tableti iliyokikazi zaidi katika utambulisho wa tableti hii afisa Panos Panay wa Microsoft alisema, “Hii ndiyo tableti inayoweza kuondoa umuhimu wa kuwa na laptop”.

Microsoft Surface Pro 3 kioo

Upana wa Surface Pro 3 (kushoto) – Surface Pro 2 (kulia)

Surface Pro 3 Intel Core i3 inapatikana kwa bei ya dola za kimarekani 700 (Takribani Tsh 1,160,000) na kwa uwezo mkubwa zaidi bei inapanda zaidi.

SOMA PIA  Windows 10; Kwa nini ni bora zaidi na uipate kabla muda wa BURE kuisha! #DoMore

Uwezo/Sifa

  • Intel Core i3, i5 na i7
  • Inakuja Peni ya kidigitali
  • Kava lenye ‘Keyboard’ (Type Cover)
  • USB Port
  • Sehemu ya kuweka kadi ya diski (Card Reader)
surfacepro3cover

Kava zilizotengenezewa na Keyboard yenye ubora zaidi ukilinganishi ya ile ya Surface Pro 2

new cover hinge

Uwezo Mzuri wa Kutumiwa Mahali Popote

Je Microsoft watafanikiwa katika kuongeza mauzo ya tableti zao? Muda utaonesha…

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania