fbpx
Gemu, Microsoft, Teknolojia

Xbox Series S Console: Kuzinduliwa Novemba 10

xbox-series-s-console-kuzinduliwa-novemba-10
Sambaza

Microsoft, watengenezaji wa vifaa vya kuchezea magemu vya XBox wametangaza rasmi ujio wa Xbox Series S pamoja na bei yake.

Microsoft wamesema toleo hilo jipya la Xbox litaingia sokoni Novemba 10 mwaka huu. Kwenye suala la bei itaanzia dola 299 za Kimarekani – takribani Tsh 700,000/=.

XBox Series S inakuja katika rangi nyeupe na inachukua sifa ya kuwa Xbox yenye umbo dogo zaidi, urefu wa inchi 10.8 na upana wa inchi 2.5.

INAYOHUSIANA  Samsung kuja na simu inayofunguka kwa nje
Xbox Series s
Xbox Series: Kuzinduliwa Novemba 10 pamoja na toleo lingine la Xbox Series X

 

Vingine:

  • Inakuja na port mbili za USB.
  • Port ya HDMI na Ethernet – kwa ajili ya intaneti.
  • CPU ya 3.6GHz, yenye uwezo wa kuhimili uchezaji magemu wa kiwango cha HD cha 1440p na 60fps na zaidi.
  • Diski ujazo wa GB 512 pamoja na RAM ya GB 10

Microsoft wanasema Xbox Series S inauwezo wa mara tatu zaidi katika ufanisi ukilinganisha na Xbox One X.

INAYOHUSIANA  Google yaongezwa kwenye SwiftKey

Zitaanza kupatikana kuanzia Novemba tarehe 10, ila wanaoweza kufanya malipo ya kabla basi wanaweza kuanza kulipia (pre-order) kuanzia Septemba 22.

Je una mtazamo gani juu ya toleo hili la Xbox?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Richard Kiwanga

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*